Ligi Kuu Uingereza imeendelea usiku wa December 21 kwa mchezo mmoja kupigwa katika dimba la Emirates, Arsenal waliikaribisha Manchester City
katika dimba hilo. Huu ndio mchezo uliokuwa unavutia zaidi kuliko mechi
zote za Uingereza zilizopigwa weekend ya December 19 na 20.
Mvuto wa mchezo huu unakuja kutokana na
timu zote kuwa katika nafasi tatu za juu, hivyo ushindi kwa kila timu
ulikuwa ni muhimu kwani utakuwa unamuweka karibu na Leicester City inayoongoza. Hata hivyo kwa takwimu za mechi tano za mwisho kukutana kati ya Arsenal dhidi ya Man City, Arsenal inaonesha kuwa na rekodi nzuri.
Kwani imeshinda mechi mbili kati ya tano dhidi ya Man City, imetoka sare mbili na kufungwa mechi moja. Takwimu zilizidi kuwa rafiki kwa Arsenal baada ya dakika ya 33 Theo Walcott kupachika goli la kwanza kwa Arsenal, huku mambo yakizidi kuwa mabaya kwa Man City. Lakini nyota wa Arsenal Mesut Ozil mfalme wa assist ndio aliotengeneza magoli yote mawili ya Arsenal.
Arsenal kupitia kwa mshambuliaji wake wa kifaransa Oliver Giroud alipachika wavuni goli la pili dakika ya 45 na kuufanya mchezo kumalizika kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Man City, huku goli la Man City likifungwa na Yaya Toure dakika ya 82. Kwa matokeo hayo Arsenal wanakuwa nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi wakiwa na jumla ya point 36 tofauti ya point 2 na Leicester City wanaoongoza Ligi.
0 comments:
Post a Comment