Kama vile ambavyo kuna mashindano ya
watu wenye sura nzuri, mvuto, warembo, na mashindano mengine yote
tuliyozoea, kuna mashindano ya wenye sura mbaya pia toka Zimbabwe.
Jamaa anaitwa Maison Sere,
hana kibarua chochote rasmi kinachomuweka mjini lakini kagusa kwenye
stage inayohusu mashindano ya watu wenye sura mbaya na kaibuka na
ushindi wa dola 500 mkononi kama utani yani !!
Unaambiwa kwenye mashindano hayo, William Masvinu
ni jamaa ambaye amewahi kushinda Taji hilo mara tatu
mfululizo amelalamika kwamba kumefanyika upendeleo ndio maana safari hii
amelikosa taji hilo na kujikuta akishika nafasi ya pili, anachoamini ni kwamba kwa ubaya wa sura yake anastahili #1.
Maison Sere
hana meno kadhaa mdomoni, na amefanikiwa kuibuka na ushindi huo kwa
kuwashinda washiriki wengine watano huku akijikunjia na mkwanja wake
dola 500 ambazo ukizichenji zinagusa kama Milioni 1 hivi !!
Stori yake imegusa vichwa vya habari vya Kimataifa pia, unaweza kucheki ripoti yake kutoka kituo cha TV ya China CCTV.
0 comments:
Post a Comment