Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Laurence Masha,
ambaye hivi karibuni amejiunga na chama cha upinzani cha Chadema
akitokea CCM leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini Dar
es Salaam.
Akiwa mbele ya Hakimu Waliyarwande Lema, Masha amesomewa shtaka la kutoa lugha ya matusi kwa Afande Juma Mashaka jana jioni katika kituo cha polisi cha Oysterbay Jijini Dar es Salaam alipoenda kuwawekea dhamana vijana 17 wa kundi maarufu la linalojulikana kwa jina la Kingereza kama 4U Movement.

Mshtakiwa Masha alikana shtaka hilo, na kupewa sharti la dhamana ya
shilingi milioni 1 pamoja na wadhamini wawili, lakini alishindwa
kutimiza masharti ya dhamana kutokana na muda wakazi kuisha na
kurejeshwa rumande. Kesi yake itatajwa tena tarehe 7 mwezi ujao.
Vijana 4U Movement walikamatwa jana katika barabara za Morocco na Ali Hassan Mwinyi, wakituhumiwa kuvaa fulana zinazodaiwa kukashifu chama tawala cha CCM, zilizoandikwa maneno haya, “Watanzania Hawa Wanataka Mabadiliko, Wasipoyapata Ndani ya CCM, Watayatafuta Nje ya CCM”. Maneno waliyoyatoa katika moja ya hotuba za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
source EATV

0 comments:
Post a Comment