Eugene Mwaiposa enzi za uhai wake.
MBUNGE wa Jimbo la Ukonga, Eugene Mwaiposa (CCM) amefariki dunia
akiwa nyumbani kwake mkoani Dodoma leo baada ya kusumbuliwa na shinikizo
la damu kwa muda mrefu.
Taarifa iliyotolewa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ni kwamba marehemu alikuwa na tatizo la shinikizo la damu kwa
muda mrefu na amefariki akiwa nyumbani kwake Dodoma.
Ameongeza kuwa nyumbani kwa marehemu ni eneo la Chaduru jirani na jengo jipya la Hoteli ya Shabiby barabara ya Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.
Shughuli ya kuaga mwili itafanyika kesho. Naibu Spika ametumia kanuni
ya 152 kuahirisha bunge hadi keshokutwa Alhamisi kutokana na msiba huo.
Related Posts:
KESHO NI SIKU YA NYERER,TUMUENZI KWA VITENDO,AMANI,UPENDO NA MSHIKAMANO &… Read More
HASHIM THABITMCHIZI NI MTANZANIA ANAWAKILISHA VYEMA KWA OBAMA MAREKANI KATIKA MPIRA WA KIKAPU...HALLA MA MEN … Read More
CHECK MACHIZI WA KILI FM
MCHIZI ANAITWA KENNEDY ROWLAND A.K.A K ROW;MCHIZ ANAFANYA VIPINDI KIBAO ILA ZAIDI NI KIPINDI CHA MICHEZO A.K.A KILI SPORTS. MSOME KILA SIKU KUANZIA SAA MBILI NA NUSU HADI SAA TAT… Read More
NIAJE MAZEE!!!!!SWAGA ZIPO ON MAZEE....MCHIZI NIMEJI COMMIT KUKUWEKA UPDATED NA KILA ISHU ITAKAYOTOKEA AMBAYO UNAPASWA KUIJUA.KAMA WE NI MJANJA BAS NJOO NDANI… Read More
MAZEE MNAZUNGUMZIA VIPI BABU FEGI KUMZINGUA ROONEY,NDIO UZEE ?… Read More
0 comments:
Post a Comment