Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu
Sixtus Mapunda pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Tanzania
kwenda kumzika marehemu Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi.
Mke wa Marehemu Kapteni John Komba ,Salome (kushoto) akiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
akiweka shada la maua pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete juu ya kaburi
la Kapteni John Komba aliyezikwa kwenye makaburi ya kijiji cha Lituhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima mara baada ya kuweka
shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Komba.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua
kwenye kaburi la Kapteni John Damian Komba aliyezikwa kijijini kwake
Lituhi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Lameck Mchemba pamoja na Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye wakiweka shada la maua
juu ya kaburi la Kapteni John Komba aliyefariki jijini Dar es Salaam
tarehe 28 februari na kuzikwa kijijini kwake Lituhi tarehe 3 Machi 2015.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu (kulia) akiweka shada la maua pamoja na mkewe kwenye kaburi la Kapteni John Komba.
Khadija
Kopa akiwa katika huzuni kubwa mara baada ya kuweka shada la maua kwenye
kaburi la Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi.
0 comments:
Post a Comment