Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Wednesday, March 4, 2015

CHEKA NA UNCLE KITIME:NIKICHAGULIWA KUWA MKUU MTAIPATA HAPA MJINI


WE ACHA TU kuna vitu najua Mungu anajua akivipitisha kwangu itakuwa shiiidaaaa. Kwa mfano ikitokea nipate zali la mentali, Mkuu akiamua kunichagua kuwa Mkuu wa Wilaya, hapo jueni kabisa ntakuwa na vipaumbele vya muda mfupi na muda mrefu.
Na hivi vya muda mfupi nitahakikisha kuwa lazima nivitekeleze ile wiki ya kwanza tu ya kukabidhiwa rungu. Niwe mkweli kipaumbele cha kwanza kitakuwa ni kumshughulikia mama mwenye nyumba wangu. Unajua huyu mama ananinyanyasa sana kwa kashfa zake ambazo zinanifanya niwe namuogopa nikimuona nanywea kama kuku kanyeshewa mvua.
Kila tukipishana ananikumbusha jinsi nilivyo maskini  wa kutupwa nisiye na mbele wala nyuma, eti ndiyo maana napanga kwake na hata kodi inanishinda. Kwa hiyo ile nikitangazwa tu kuwa nimechaguliwa, huyu mama nitamuweka ndani kwa kosa la kutukana kiongozi wa ngazi za juu.
Hicho ndicho kipaumbele changu cha kwanza, pia nitapita dukani kwa Mangi kumtangazia kuwa kama alikuwa ananidai deni limefutika, habari ndiyo hiyo. Lazima nitafute suti kali na kuanza kupitia vijiwe vya washkaji wote niwape taarifa kuwa kuanzia sasa lazima waniamkie shikamoo, ukiwaachia hawa wanaweza kujiona eti wao nao taip yako!
Sasa naona ni muhimu hapa nitoe ushauri kwa yeyote atakayechaguliwa wadhifa kama huu ni vitu gani muhimu kufuata.  Kwanza ni kuwahi kufanya mambo yetu yale ya Kiafrika, bila utamaduni, utaadhirika mapema sana, hivyo ni muhimu kutengeneza kinga kuzuia watu wenye roho mbaya.
Hapa inahitajika kupata mganga mzuri, mnaweza kunitafuta niwaunganishe kwa babu yangu, maana babu ni kiboko. Kwanza babu atakuchemsha kwenye chungu kimoja kikubwa hii ni kusafisha nyota, ukiwa na nyota safi unakuwa na uwezekano wa kupanda cheo harakaharaka, baada ya hapo atakuchanja chale ili wabaya wakituma makombora yasikupate tena yawarudie, si unajua mswahili alivyo, asikuone umepata ataanza kutafuta kila njia ukikose.
Baada ya hapo utapata dawa za kukufanya watu wakusikilize, unajua bila hizi dawa ukiwa unatoa amri utakuta watu hawajali sasa hapo unakuwa mkubwa feki, hii mara nyingi inakuwa hirizi ya kuvaa shingoni. Kisha babu atakupa hirizi za kuhakikisha huondolewi kwenye cheo chako, hirizi hizi utaziweka sehemu kadhaa, moja unavaa mkononi, nyingine unaiweka kwenye kiti ofisini kwako, jingine kwenye gari, nyingine utafukia kwenye geti la nyumba mpya utakayopewa.
Kisha utakuwa na hirizi ya kuvaa kiunoni, hii ni muhimu ili kukiwa na vikao vya kamati mbalimbali watu wote wanakusikiliza wewe tu. Ni muhimu kuwa na hirizi nyingine ya kutembea nayo kwenye pochi kulinda pesa unazopata zisichukuliwe na chuma ulete, ukajikuta mshahara unapata lakini haukai.
Kikubwa ni muhimu kuhakikisha unarudi kwa Babu kila baada ya mwezi kufanya maboresho ya hizi kinga, maana lazima ujue maadui wakikujaribu wakiona wamekwama wanaenda kuongeza ufundi hivyo muhimu kuboresha  kinga hizi.Nategemea kupata simu kwa wingi kwa wahusika ili kuweza kuboresha ulinzi huu shirikishi!

0 comments: