Ajuza
raia wa japan Misao Okawa (117) akiwa na familia yake. Ajuza huyu bado
yupo katika afya njema na hata msosi anaupiga kama kawaida.
Ajuza
raia wa japan Misao Okawa (117) leo amefanya Birthday yake ya kuzaliwa
akiwa 117 akiwa ndiye mtu aliyekula chumvi nyingi duniani.
Okawa aliyezaliwa Machi 5, 1898 ameifurahia siku yake hiyo akiwa na familia yake.
Akizungumza Misao Okawa amesema kuishi miaka 117 sio kitu alicho kizania.
Ajuza
huyo sasa analelewa katika kituo maalum cha wazee kilichopo katika mji
wa Osaka na wahudumu katika kituo hicho wanasema kuwa, Okawa katika
miezi ya karibuni amepunguza uwezo wake wa kusikia.
Ajuza huyo alifunga ndoa mwaka
1919 na Yukio ambaye alifariki mwaka 1931 wakiwa wamezaa watoto watatu
kati yao wasichana wawili na mvulana mmoja ambapo sasa anawajukuu wanne
na vitukuu 6.
Alitambuliwa
rasmi kuwa ndiye mtu mzee kuliko wote duniani mwaka 2013 na kitabu cha
kumbukumbu Duniani cha Guinness.Source: BBC-UK
0 comments:
Post a Comment