Katika hali isiyokuwa ya kawaida, watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino),
wamepigana ngumi na mateke wakigombea kuingia kumwona Rais Jakaya
Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam. Tukio hilo la aina yake lilitokea
jana majira ya saa nne asubuhi ambapo lilianzia kwenye eneo la mapokezi
Ikulu mara baada ya walemavu hao kukaguliwa na kuwekwa kwenye chumba
maalumu cha kupumzikia wageni. Baada ya muda, ofisa wa Ikulu alifika
kwenye chumba walipokuwa walemavu hao akiwa na karatasi yenye orodha ya
watu 15, ambao ndio waliopaswa kumwona Rais. Kila ofisa huyo alipokuwa
akisoma jina, mhusika alitoka nje ya chumba hicho tayari kwa kwenda
kumwona Rais. Baada ya ofisa huyo kumaliza kusoma majina hayo, alisema:
“Hawa ndio wanaokwenda kuwawakilisha kwa sababu hamuwezi kuingia kundi
lote hili.”
Wale wengine walioachwa hawakukubaliana na hali hiyo basi vurugu ndio likaanzia hapo!
0 comments:
Post a Comment