Hamida Hassan na Gladness Mallya BAADA ya kuficha kwa muda mrefu huku akikanusha kujifungua, hatimaye staa wa muziki wa mduara na sinema za Kibongo, Snura Mushi ‘mama wa Hawashi’ ameamua kumwanika ‘live’ mwanaye aliyejifungua hivi karibuni na kutoa sababu kuu ya kufanya hivyo.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, nyumbani kwake Mwananyamala, Dar, Snura alisema kuwa yupo tayari kuonekana mbaya kusemwa lakini sababu kubwa ya kumficha mtoto wake ilikuwa ni kazi yake ya muziki ambayo anaitegemea kama baba wa familia yake.
“Ikumbukwe kuwa mimi ndiye baba na ndiye mama wa watoto pamoja na familia yangu hivyo nililazimika kuficha kwa nia ya kuwaweka mapromota wangu ambao kama ningetangaza nina mimba wasingenipa kazi kabisa na huwezi kuamini nilikata nyonga mpaka nikiwa na miezi mitano ya ujauzito,” alisema Snura.
Snura alitiririka kuwa kwa kawaida, kwa Tanzania, mwanamke akiwa na ujauzito hasa muimbaji, kumpa kazi huwa ni vigumu hivyo alilifikiria hilo kwa upana akaona hawezi kupata kazi haraka kwani kila atakayemtaka ataambiwa ana mimba au amejifungua.“Kwa sasa nimeshakuwa fiti ‘so’ nimeamua kuweka wazi kwani nina uwezo wa kufanya kazi wakati wowote nikiitwa,” alifunguka Snura.
AKUBALIANA NA MENEJA WAKE
Alisema: “Baada ya kuona siwezi tena kupanda jukwaani, nilikaa na kumpa wazo meneja wangu (HK), tukapanga nikiuliziwa aseme nimeenda Afrika Kusini kufanya video yangu lakini ukweli nilijifungia chumbani nyumbani kwangu, chumba kilipewa jina la kwa Madiba.
AJIFUNGULIA PALESTINA
“Nilijifungua katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza, Dar. Ilikuwa Januari 2, 2015. Niliingia nimevaa nikabu na niliwatonya manesi kuwa nahitaji chumba cha peke yangu. Kweli walinikubalia, nawashukuru sana kwa hilo, nilipata mtoto wa kiume anayeitwa Taltham.”
MASTAA WALIOMFICHIA SIRI
Snura aliwataja mastaa waliomfichia siri na kuwashukuru kuwa ni Halima Yahya ‘Davina’ aliyefanyia arobaini nyumbani kwake, Tundaman, Amisuu Malick na wengine wachache.
Mwisho Snura aliwaomba Wabongo wamsamehe kwa kuwa alifanya hivyo kwa sababu ya kazi na amewaomba mapromota wamtafute kwani kwa sasa amekuja upya na mambo mapya huku akiwataka mashabiki watembelee ukurasa wa mtoto wake wa Instagram kwa jina la Tsnura kwa ajili ya kujionea picha zinazomuonesha kuanzia mimba mpaka mtoto alivyozaliwa.
0 comments:
Post a Comment