Na Timu ya Championi,Dar es Salaam
PIGO MOJA! Hiyo ndiyo lugha inayotamkwa na mashabiki wa Simba na Yanga hivi sasa kuelekea mechi yao ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa timu hizo, wanaamini ushindi wowote watakaoupata utakuwa ni pigo moja takatifu kwa timu pinzani, ambalo litaifanya iwe chali kabisa. Yanga wanataka kuipiga Simba na Simba nao wanataka kuipiga Yanga. kazi ipo! Lakini jibu litapatikana kesho Taifa.
Timu hizo zilipokutana katika mechi ya ligi kuu mzunguko wa kwanza, zilitoka suluhu wakati huo Yanga ilikuwa ikifundishwa na Mbrazili, Marcio Maximo huku Simba ikinolewa na Mzambia, Patrick Phiri ambao wote wametimuliwa kwa sababu mbalimbali.
Yanga itamvaa mtani wake wa jadi ikiwa inaongoza kwenye msimamo wa ligi kuu na pointi zake 31 ikifuatiwa na Azam FC yenye 27 huku wapinzani wao Simba wakiwa na 23.
Katika mechi hiyo, Yanga wataingia uwanjani wakiwa na matumaini ya ushindi na kujiamini kutokana na matokeo mazuri katika mechi za ligi kuu na Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwaondoa katika michuano hiyo, BDF XI ya Botswana.
Simba wenyewe wataingia uwanjani kwa kujiamini baada ya kupata ushindi katika mechi ya mwisho ya ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons waliyoifunga mabao 5-0 yaliyofungwa na Ibrahim Ajibu aliyepiga ‘hat-trick’ huku Emmanuel Okwi na Ramadhani Singano ‘Messi’ wakifunga moja kila mmoja.
Kambi
Timu hizo, kila moja imejichimbia nje ya Dar, kwa upande wa Simba, wao wameweka kambi ya pamoja huko visiwani Zanzibar huku Yanga wakiweka Bagamoyo, Pwani.
Watakaokosekana
Katika mechi hiyo, Yanga wanatarajiwa kumkosa kiungo wao mshambuliaji Mbrazili, Andrey Coutinho anayesumbuliwa na majeraha ya goti na beki wa pembeni, Juma Abdul mwenye kadi tatu za njano huku kikosi cha Simba kikiwa fiti kwa ajili ya mchezo huo.
Tambo za makocha
Kwa upande wa Kocha wa Simba, Goran Kopunovic, alisema: “Licha ya timu yangu kuwa nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu, sioni sababu ya kupoteza mechi dhidi ya Yanga kutokana na uimara wa kikosi changu kwa kuwa ninajua wapinzani wangu wanaongoza ligi, hivyo ninaahidi kupambana ili tupate matokeo mazuri.”
Kwa upande wa Pluijm alisema: “Morali ya wachezaji wangu kiukweli ipo juu sana, nina matumaini makubwa ya ushindi katika mechi hii, ninajua ushindani utakuwa mkubwa kutokana na upinzani uliopo kila zinapokutana.”
Matajiri waMWAGA MAMILIONI KAMBI YA YANGA
Juzi mabosi wa Yanga walitia timu kwenye kambi ya kikosi hicho iliyopo Bagamoyo wakiongozwa na makamu wake mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro, Seif Ahmed ‘Magari’, Mohammed Binda na Abdallah Bin Kleb ambapo walitoa ahadi ya fedha isiyopungua milioni 40 iwapo wataifunga Simba, kesho.
MABILIONEA WAWILI SIMBA WATUA KUTOKA ULAYA, WATANGAZA NEEMA
Taarifa kutoka kwa chanzo chetu ndani ya Simba zinasema mabilionea wawili Watanzania (majina tunayo) wanatua jijini Dar leo kutokea Ulaya kikazi na moja kwa moja wataelekea kwenye mazoezi ya kikosi hicho na kuwatangazia dau nono wachezaji endapo wataifunga Yanga.
Tambwe, Ngassa waagizwa mabao
Kocha Hans van Pluijm amewapa jukumu zito washambuliaji wake, Amissi Tambwe na Mrisho Ngassa kuhakikisha hawafanyi ajizi kwa kufunga mabao ya mapema ili kuwachanganya wapinzani.
Simba yashtukia janja ya Yanga
Uongozi wa Simba umedai kuwa umeshtukia ujanja unaofanywa na Yanga wa kuhusiana na wao kumchezesha mshambuliaji Ibrahim Ajib kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons huku akiwa na kadi tatu za njano na kwamba kelele zao haziwasumbui hata kidogo.
Umesema kelele hizo zilikuwa na lengo la kuwatoa mchezoni vijana wao lakini wameshtukia na wameshawajenga kisaikolojia, hivyo kila kitu kipo sawa kwa sasa.
Tambwe aomba ulinzi, kufanya maajabu
Tambwe ambaye anacheza kwa mara ya kwanza mchezo wa watani akiwa ndani ya Yanga, ameiomba TFF kuhakikisha inawaagiza waamuzi wake wachezeshe kwa kuzingatia sheria 17 za soka.
Aliongeza: “Nimejipanga vizuri sana na nina matumaini makubwa ya kufanya maajabu katika mechi hiyo ambayo naamini itakuwa na ushindani mkubwa hasa kwa upande wangu.”
Phiri amwonea huruma Kopunovic
Patrick Phiri ambaye alikuwa kocha wa zamani wa Simba, ametoa ya moyoni huku kubwa akidai anamuonea huruma mrithi wake kwani ni moja kati ya mechi ngumu na kila jicho la Mwanasimba linamuangalia yeye.
Anasema: “Nilipokuwa nikiiongoza Simba nilikuwa nikipata wakati mgumu sana pindi tulipokuwa tukikutana na Yanga, kwani kila mtu jicho lake lilikuwa juu yangu.”
Cannavaro amruhusu Ajibu acheze
“Nani wa kumuogopa Ajibu Yanga, kiukweli sijaona kabisa kutokana na ubora wa safu yetu ya ulinzi, ukiangalia mabeki wana ubora mkubwa wa kupamba na mabeki zaidi ya huyo Ajibu.
“Sioni sababu ya kuongea sana, tungoje tu hiyo mechi ya Jumapili tuone, tumekabana na washambuliaji wangapi atusumbue huyo Ajibu!”

0 comments:
Post a Comment