MOJA KWA MOJA KUTOKA TAIFA; SIMBA 0 VS YANGA 0
Dk 1 Mechi imeanza kwa kasi na Yanga wanakuwa wa kwanza kupata kona, lakini haina kitu
Dk 2, Ibrahim Ajib anakuwa wa kwanza kupiga shuti kali lakini linapita pembeni mwa lango la Yanga.
Dk 8, Msuva anaingia kwa kasi, anamzidi mbio Mohammd Hussein na kupiga shuti dhaifu.
Dk 9, Yondani anafanya kazi ya ziada kumzuia Okwi na kuondoa mpira huo.
Dk 14, Cannavaro anamuangusha Okwi aliyekuwa anakwenda langoni mwa Yanga lakini faulo aliyopiga Okwi inaishia miguuni mwa wachezaji wa Yanga.
Dk 18, Msuva anaingia vizuri ndani ya eneo la 18 ya Yanga, lakini Murishid anaokoa.
Dk 19, Tambwe anapiga kichwa mbele ya Murishid na mpira unapita juu ya lango la Simba
Dk 21, Mwamuzi Said Juma Makapu analambwa kadi ya njano.
Dk 24, Mrwanda na Kessy wanalambwa kadi za njano kutokana na faulo na kuchezeana kibabe.
Dk 27 Singano anagongana na kipa Barthez, sasa anatibiwa...
MABADILIKO DK 30, Yanga wanamtoa DANNY MRWANDA na HUSSEIN JAVU anachukua nafasi yake
KADI 34 Saanya anatoa kadi za Njano kwa Banda na Yondani
Dk 36, Ivo anaokoa mpira miguuni mwa Ngassa anabaki Msuva peke yake na mpira anashindwa kulenga lango.na GOLI BADO NI 0-0
Dk 41, Tambwe anaingia katika eneo la hatari la Simba na kupiga shuti lakini linatua kwa ulaini katika mikono ya Ivo Mapunda.
KADI Dk 42, Niyonzima anamuangusha Singano na kupewa kadi ya njano
DK 45 Tambwe anaweka kifuani vizuri anamuachia Msuva lakini anapaisha juu
DK 43 anapiga faulo Okwi inatoka kidogo nje ya lango la Yanga
MAPUMZIKO:
DK 47 Yanga wanaingia vizuri katika eneo la hatari la Simba, Tambwe anashindwa kuuwahi mpira, Murishid anaondosha
KADI Dk 49 Nadir Haroub 'Cannavaro' analambwa kadi ya njano kwa kumkata Ibrahim Ajib
GOOOOOOOOO Dk 52, Okwi anaifungia Simba bao baada ya kumchungulia Barthez aliyekuwa mbele ya lango na kupiga mpira mrefu unaojaa moja kwa moja nyavuni.
Dk 61, Ajibu anapata nafasi nzuri katika ya lango la Yanga baada ya mabeki wa Yanga kugongana lakini 'anaichezea' kwa kupiga shuti kuuubwaaaa.
Dk 60 Yanga wanapata kona lakini Simba waokoa kwa ulahisi
Dk 53 hadi 56 mpira zaidi unachezwa katikati huku Yanga wakionekana kupania zaidi.
Dk 62 hadi 64, kidogo ni mpira unakuwa wa matukio, wachezaji wanasukumana, Okwi anafanyiwa madhambi na Twite, anatolewa nje kutibiwa na nje inaonekana Kpah Sherman anaonekana akipasha.
Dk 70, Javu anamtoka Kessy na kupiga shuti kali ambalo Ivo anaookoa.
Dk 77 anatoka Ngassa nafasi yake inachukuliwa na Kpah Sherman
Dk 75, Simba wanamtoa Ibrahim Ajibu anaingia Elius Maguri.
KADI NYEKUNDU Dk 74, Niyonzima anapewa kadi ya pili ya njano inayozaa nyekundu. Alifanya kosa la kuupiga mpira kwenye nyavu za Simba baada ya mwamuzi Saanya kuwa amepuliza filimbi lakini yeye akaubutua mpira.
Dk 80, Okwi anapiga shuti jingine kali lakini linapita juu kidogo ya lango la Yanga
Dk 84, cannavaro anacheza vizuri na kumzuia Messi aliyepigiwa pasi nzuri na Okwi
Dk 87 Yanga wanapata kona baada ya shambulizi langoni mwa Simba
Dk 89, Maguri anapiga kichwa safi mbele ya mabeki wa Yanga na Barthez anafanya kazi nzuri na kuokoa.
Dk 90+3Simba wanamaliza mpira kwa kupiga pasi zaidi ya 28 bila ya kupoteza hadi mwamuzi Martin Saanya alipomaliza mpira
na MPIRAA UMEKWISHAA SIMBA WANAIBUKA KWA USHINDI WA BAO 1-0
0 comments:
Post a Comment