Bondia
nyota zaidi nchini, Francis Cheka amerejea uraiani baada ya mahakama
kutengua kifungo chake cha miaka mitatu jela badala yake atatumikia
adhabu yake hiyo akiwa nje ya gereza.
Cheka ameachiwa leo Jumanne baada ya kushinda rufaa yake aliyokata kupinga
kifungo cha miaka mitatu gerezani.
Tayari Cheka alianza kutumikia kifungo hicho mjini Morogoro.
Lakini taarifa za uhakika zinasema ameachiwa leo baada ya kushinda
rufaa hiyo.
“Tayari ameachiwa, lakini tunashughulikia masuala kadhaa kumalizia
ishu hiyo. Ila tayari yuko nje,” alisema Kaike Siraju, promota wa ngumi za
kulipwa aliyekuwa akipambana kuhakikisha Cheka anatoka.
Cheka alihukumiwa kwenda jela baada ya kumtwanga na kumuumiza meneja
wa baa yake mjini Morogoro akimtuhumu kumsababishia hasara.
0 comments:
Post a Comment