Fulana iliyozua utata |
Rihannaameshinda kesi ya madai dhidi ya duka la mavzi la Topshop juu ya fulana iliyobandikwa sura yake.
Lakini katika kile kinachoonekana kama maamuzi muhimu ilibidi yachukuliwe kuzuia uuzwaji wa fulana hizo za kata mkono.
Duka hilo kubwa lilijitetea kuwa limekuwa likichapisha sura za wasanii miaka kadhaa iliyopita katika fulana na Rihanna si wa kwanza,wapo waliotangulia kama Elvis Presley, Jimi Hendrix na Prince.
Kutokana na hali hiyo Geoffrey Hobbs wakili anayetetea duka hilo anadai kuwa kuwazuia kutouza bidhaa hiyo ni matumizi mabaya ya sheria .
Bwana Hobbs ameongeza kwamba jamii haiamini kwamba kila sura ya mtu maarufu unayoiona katika vazi basi imepewa ruhusa na mhusika,hata hivyo Rihanna ameshafanya biashara na kupata faida kubwa na maduka makubwa ya mavazi kama Topshop wenyewe na mpinzani wake River Island.
Hakuishia hapo katika kukosoa hukumu hiyo ya maahakama kuu kwamba watu maarufu hawana mamlaka ya kuingilia kazi zao za uzalishaji na Topshop walipoamua kutumia sura ya mwanamuziki huyo haina maana kuwa wamempitia tu lah.
Hukumu hiyo inadaiwa ilikuwa imeangazia na kulinda hadhi na heshima ya msanii huyo asije akaharibiwa nia yake njema katika tasnia ya mavazi.
0 comments:
Post a Comment