HABARI
wadau wa safu yetu, tupo tena pamoja katika kujuzana jinsi gani maisha
ya kimapenzi yalivyo.Watu wengi wanajaribu kupata jibu hili kila siku huku mahusiano mengi yakiendelea kufa kibudu.Hii ni kutokana na ukweli kwamba kutokana na utandawazi
ulivyo na mila na desturi zetu Mwanaume na mwanamke wamekuwa na nafasi sawa za kumbelelezwa katika mahusiano_na hii inapelekea jinsia flani kuamini kwamba ni jukumu la mwenzake kulinda pendo lao:LAKINI JE NI NANI AMBAYE ANANAFASI ZAIDI YA KULINDA PENDO kati ya mwanaume na mwanamke?
.
Maandiko mengi yamekuwa ni kama ya kuonyesha kuwa mwanamke ndiye mwenye
dhamana kubwa ya kuamua juu ya penzi au ndoa aliyomo. Ingawa ni kweli
kuwa kuna umuhimu mkubwa wa mama kuwa mshirika muhimu katika ndoa,
lakini amini usiamini, mwanaume ndiye hasa mwenye kushika turufu ya
penzi linalohusika.
Na ninasema hivi hasa kutokana na ukweli ambao nafsi zote mbili
zinakubaliana kuwa mwanaume ndiye kichwa cha nyumba. Usemi huu unaweza
kuonekana ni mwepesi kama utaangaliwa kwa upande mmoja tu, ambao
kimsingi unabeba maana ya uwajibikaji juu ya majukumu ya kuilea na
kuilinda familia.
Na unapozungumzia kuhusu jambo hili, akili ya kawaida na haraka, ni juu
ya wajibu wa mume au baba katika kuhakikisha familia inapata huduma zote
muhimu kama chakula, malazi, matibabu, masomo na kadhalika.
Ni kweli. Lakini maana halisi ya kichwa cha nyumba ni kuwa huyu ndiye
kila kitu. Wote tunajua, binadamu anaweza kukosa mikono na miguu, lakini
akaendelea kuitwa mtu kwa sababu tu, anacho kichwa. Bila kichwa, kiumbe
hicho kitaitwa jina lingine lisilo binadamu.
Uzoefu unaonyesha, uharibifu wa ndoa au uhusiano mwingi wa kimapenzi,
huanza kupata msukosuko baada ya baba kuanza kutoka nje ya mstari. Nje
ya mstari hakumaanishi kushiriki mapenzi, bali hata kuacha kutekeleza
baadhi ya majukumu yake. Baba, kwa sababu zozote, anapozembea au kukataa
kulipa ada ya mtoto, ni wazi kuwa atamfanya mama kuanza kuwaza mambo
mengi hata yaliyo nje ya uwezo wake.
Lakini
hata ile ya mapenzi yenyewe, ni mwanaume ndiye mwenye wajibu mkubwa.
Kama baba atakuwa ni mtu mwenye furaha muda wote, litakuwa ni jambo la
kushangaza sana kumuona mama akinuna. Yapo makosa madogomadogo ambayo
wote huyafanya, wakati mwingine kwa bahati mbaya au kutojua.
Lakini kinachotokea kuharibu hali ya hewa ni kwa mmoja wao kuamua
kulichukulia jambo hilo dogo kwa tafsiri yake, lakini kwa ubaya na
inakuwa mbaya zaidi kama huyu atakuwa ni mwanaume. Imetokea kwa mfano,
mmoja wa wapenzi amekwazwa na tabia ya mmoja wa wazazi wa mwenzake.
Katika kulizungumzia jambo hili, yule ambaye wazazi wake wanatuhumiwa,
kwa makusudi au kwa bahati mbaya, anaweza kusema; ‘kama huwapendi wazazi
wangu basi achana na mimi’.
Hii ni kauli ambayo hakuna yeyote angependa kuisikia, lakini kwa kuwa
kulikuwa na mazungumzo yaliyotangulia, ni wazi kuwa kitu kikubwa
kinachotakiwa ili kuondoa mzozo, ni busara. Kama mnunaji ni mama, ni
rahisi baba kumbembeleza na pengine kwa kutumia mamlaka yake, anaweza
kulipooza jambo hilo.
Lakini naona kabisa jinsi gani suala hilo linaweza kuwa kubwa kama baba
ndiye atavimba mashavu kwa hasira baada ya kauli kama hii. Na labda
ieleweke kuwa siyo nia yangu kutetea nafasi ya mwanaume katika uhusiano
wa kimapenzi, lakini kama tunataka mambo yetu kwenda sawa, daima lazima
tuwe tayari kukubaliana na ukweli, hata kama unatuumiza.
Kwa hiyo, nimalizie tu kwa kuwasihi wababa, kama wenyewe hawawezi kusoma
hapa na kuelewa ujumbe ninaowatumia, basi akina mama waonyesheni hapa
wasome, kwamba wao ndiyo wenye nafasi kubwa ya kulilea na kulienzi penzi
0 comments:
Post a Comment