Ukisikia story kwamba kumetokea wizi
katika kituo cha Polisi huwa ni story ambazo huwa zinashangaza wengi,
jiulize hivi huyo mwizi anayeiba kituo cha Polisi amejiamini kiasi gani?
Adam Wisneski alienda
kituo cha Polisi Illinois, Chicago Marekani, lengo lake ilikuwa
kuripoti tukio la kuibiwa iPhone yake akiwa ndani ya treni na baadaye
akapata mtu ambaye anaitumia akidai kwamba kauziwa simu hiyo, akamtaka
ampatie access code za simu hiyo.
Baada ya kuripoti nje akakuta baiskeli
yake haipo, akaitafuta hakuipata, ikabidi arudi ndani ya kituo hicho
tena kwa ajili ya kuripoti kupotelewa baiskeli yake.
0 comments:
Post a Comment