Habari za kuwepo kwa uhusiano mbaya kati ya nyota wa Barcelona, Lionel Messi na kocha wake Luis Enrique
mpaka sasa sio mpya masikioni mwa mashabiki wa soka barani ulaya baada
ya matukio kadhaa ambayo yamekuwa yakitokea ndani ya klabu hiyo ya Nou Camp.
Tetesi zaidi zinadai kuwa kocha Luis Enrique amepewa mechi mbili kuokoa kazi yake jambo ambalo Barcelona imekanusha lakini hakuna asiyefahamu kuwa Messi na kocha wake hawaelewani.
Chanzo cha ugomvi baina ya wawili hao
kimefahamika baada ya ripoti kadhaa toka kwa watu walioko karibu na
klabu hiyo kufichua kuwa ugomvi huu ni mkubwa kuliko inavyodhaniwa na
umefikia hatua mbaya.
Ripoti tofauti zinasema kuwa Messi
na kocha wake waligombana siku ya ijumaa wiki iliyopita na ugomvi
ulikuwa mkubwa kiasi cha wawili hao kukunjana na kutaka kupigana kabla
ya kuachanishwa na wachezaji wa Barcelona.
Messi ambaye alichelewa kujiunga na kambi ya Barcelona
baada ya kutoka kwenye mapumziko nyumbani kwao Argentina aliingia
mazoezini siku hiyo ya ijumaa na kuungana na wenzie ambao walikuwa
wakifanya mazoezi ya kucheza mechi ya wenyewe kwa wenyewe huku Enrique akiwa refa.
Katika mazoezi hayo Messi alichezewa rafu ambayo alitaka kupewa adhabu ndogo lakini Enrique hakupuliza filimbi jambo ambalo lilimkera Messi na kumfanya aanze kumshutumu Enrique.
Baada ya mazoezi hayo kumalizika Messi alimfuata Enrique na kuanza kutupiana nae maneno mpaka kufikia kukunjana kabla Neymar hajaingilia ugomvi huo na kuwatenganisha kabla hawajapigana.
Kufuatia ugomvi huu Enrique alimuacha Messi benchi kwenye mchezo uliofuata dhidi ya Sociedad na nyota huyo alijibu mapigo kwa kutohudhuria mazoezi ya jumatatu.
0 comments:
Post a Comment