Baadhi ya wachezaji wa
kikosi cha Chelsea wamewashitukiza watoto waliolazwa kwenye Hospitali ya Westminster
jijini London, England kwa kwenda kuwatembelea pia kuwapa zawadi za sikukuu ya Krismas.
Kundi la wachezaji hao
likiongozwa na nahodha John Terry waliibuka hospitalini hapo na kuanza kugawa
zawadi kwa watoto waliolazwa.
Hakuna aliyetarajia kuwa Terry pamoja na mshambuliaji Diego Costa, kipa Petr Cech na viungo Ramirez na Fillipe Luis wangeibuka hospitalini hapo kimyakimya.
0 comments:
Post a Comment