Pamoja na kuwepo na taarifa za ujio wa kocha
mpya Simba, Patrick Phiri ameendelea na mazoezi ya kikosi hicho jijini Dar es Salaam.
Phiri ameendelea kuinoa Simba licha ya kuwa
na taarifa za kwamba tayari anatakiwa kufungasha virago.
Katika mechi nane za Ligi Kuu Bara, Phiri
ameshinda moja, sare sita na kapoteza mechi moja.
Mserbia Goran Kouponovic anatarajia kutua nchini kesho kwa ajili ya kuingia mkataba na Simba.
Kocha Patrick Phiri amesema ametaarifiwa kuhusiana na kibarua chake kusitishwa.
Phiri raia wa Zambia amesema ni suala la kawaida kumtokea kocha, hivyo hana kinyongo na uongozi wa klabu hiyo.
"Wamenitaarifu kuhusiana na kuachishwa kazi, hili si jambo jipya, ingawa niliona tungeweza kubadilisha mambo.
"Najua Simba wanataka kufanya vizuri, hivyo siwezi kumlaumu mtu na utaona mwendo wa timu yetu ulivyokuwa," alisema Phiri.
Phiri amesema anasubiri kiasi cha fedha alichokuwa anadai ambacho hakueleza ni kiasi gani, halafu ataanza safari ya kurejea kwao Zambia.
"Nikimalizana nao kuhusiana na malipo yangu, nitajua lini ninakwenda nyumbani," alisema Phiri.
Nafasi yake inachukuliwa na Goran Kopunovic raia wa Serbia.
Kopunovic anaingia kwenye rekodi ya Waserbia waliowahi kuifundisha Simba akiwemo Milovan Cirkovic.
Taarifa za ndani ya Simba zinaeleza Mserbia anatarajia kuwasili nchini Jumatano
Kuponovic aliwahi kuinoa Polisi Rwanda kwa mafanikio makubwa na kuiwezesha kuwa tishio mbele ya vigogo APR na Rayon.
Nafasi ya Kocha ya Msaidizi, kuna taarifa Simba ilifanya mazungumza na na Jean Marie raia wa Rwanda aliyewahi kuipa Atraco na Rayon ubingwa wa Rwanda kwa nyakati tofauti.
Lakini hata hivyo inaonekana wameshindwa kuelewana na Selemani Matola anaendelea kuitumikia.
SOURCE:VARIOUS
0 comments:
Post a Comment