Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Thursday, November 6, 2014

NOMA:Shetta hataki tena collabo na wasanii wa ndani, ‘nafikiria kuangalia collabo International’

Shetta ni msanii ambaye karibia nyimbo zake zote alizotoa amewashirikisha wasanii mbalimbali wa nyumbani. Alimshirikisha Belle 9 kwenye ‘Nimechokwa’, Rich Mavoko kwenye ‘Sina Imani’, Dully Sykes na Tunda ‘Mdananda’, Linah kwenye ‘Bonge la bwana’ na amemshirikisha Diamond katika nyimbo mbili ‘Nidanganye’ na ‘Kerewa’.
shettaa
Alipoulizwa kupitia Power Jams ya EA Radio kama ana mpango wa kufanya collabo pia na Ally Kiba, Shetta alijibu, “Sina mpango wa kufanya collabo na Alikiba”.
“nafikiria kuangalia collabo International kwasababu nimeshafanya collabo sana na wasanii wa ndani, nafikiria sasa hivi inatosha..mawili nitoe nyimbo mwenyewe au nifanye na International artist.”
Shetta ameongeza kuwa kabla ya mwaka huu haujaisha atatoa ngoma mpya ambayo amesema kwasasa hawezi kusema kama itakuwa ni ya peke yake au collabo na msanii wa nje.

Related Posts:

0 comments: