Liverpool 0 Real Madrid 3
Ulaya, na Dunia nzima iliisubiri hii Mechi iliyochezwa Anfield kati ya Timu ambazo zimetwaa Ubingwa mara 15 kati yao, Real mara 10 na Liverpool mara 5, lakini ni Real walioibuka washindi kwa kuichapa Liverpool wakiwa kwao Bao 3-0 zilizofungwa Kipindi cha Kwanza..
Hii ni mara ya kwanza kwa Real kuifunga Liverpool katika Mashindano ya Ulaya baada ya kufungwa Mechi zao zote 3 walizokutana huko nyuma na ni Cristiano Ronaldo ndie aliefungua milango kwa kutengeneza na yeye mwenyewe kupachika Bao la kifundi baada ya kucheza ‘moja mbili’ na James Rodriguez kwenye Dakika ya 23.
Dakika ya 30, Kichwa cha Karim Benzema kiliwapa Real Bao la Pili alipounganisha krosi ya Toni Kroos na Benzema tena alifunga Bao la 3 Dakika ya 41 baada kutokea kizaazaza kufuatia Kona.
Hadi Mapumziko Liverpool 0 Real 3.
Liverpool walifanya mabadiliko wakati Kipindi cha Pili kinaanza kwa kumwingiza Adam Lallana kumbadili Mario Balotelli ambae alikuwa anapwaya.
Real waliamua kumpumzisha Ronaldo katika Dakika ya 74 wakiitizama El Clasico Jumamosi watakapocheza na Barcelona Uwanjani Santiago Bernabeu na nafasi yake kuchukuliwa na Sami Khedira.
VIKOSI:
Liverpool: Mignolet; Johnson, Lovren, Skrtel, Moreno; Gerrard, Allen, Henderson; Sterling, Balotelli, Coutinho
Akiba: Jones, Toure, Manquillo, Can, Lallana, Markovic, Lambert
Real Madrid: Casillas, Arbeloa, Varane, Pepe, Marcelo, Kroos, Modric, Rodriguez, Isco, Ronaldo, Benzema
Akiba: Navas, Carvajal, Nacho, Khedira, Illarramendi, Medran, Chicharito
REFA: Nicola Rizzoli (Italy)
KUNDI B
|
||||||||
KLABU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
+/-
|
Pts
|
Real Madrid CF
|
3
|
3
|
0
|
0
|
10
|
2
|
8
|
9
|
PFC Ludogorets
|
3
|
1
|
0
|
2
|
3
|
4
|
-1
|
3
|
FC Basel 1893
|
3
|
1
|
0
|
2
|
2
|
6
|
-4
|
3
|
Liverpool FC
|
3
|
1
|
0
|
2
|
2
|
5
|
-3
|
3
|
Arsenal walikaribia kuteketea huko Brussels, Ubelgiji lakini baada ya kuwa nyuma kwa Bao 1-0 lakini Bao 2 za Dakika 2 za mwishoni ziliwapa ushindi wa 2-1 walipocheza na Anderlecht na kumpa zawadi njema Meneja wao Arsene Wenger aliekuwa akisheherekea Miaka yake 65 ya kuzaliwa.
Arsenal walifungwa Bao Dakika ya 71 baada ya krosi ya Dennis Praet kuunganishwa na Andy Najar kwa Kichwa.
Arsenal walisawazisha kwenye Dakika ya 89 kwa Bao la Kieran Gibbs na Lukas Podolski kuwapa ushindi Dakika moja baadae.
VIKOSI:
RSC Anderlecht: Proto, Deschacht, Mbemba, Vanden Borre, Praet, Defour, Tielemans, Najar, Cyriac, Acheampong, Conté
Akiba: Roef, Colin, Kljestan, Dendoncker, Suárez, Kabasele, Mitrović.
Arsenal:Martínez, Gibbs, Mertesacker, Monreal, Chambers, Wilshere, Ramsey, Santi Cazorla, Flamini, Alexis Sánchez, Welbeck
Akiba: Huddart, Bellerín, Rosický, Arteta, Oxlade-Chamberlain, Podolski, Campbell.
REFA: Carlos Velasco Carballo (Spain)
KUNDI D
|
||||||||
KLABU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
+/-
|
Pts
|
Borussia Dortmund
|
3
|
3
|
0
|
0
|
9
|
0
|
9
|
9
|
Arsenal FC
|
3
|
2
|
0
|
1
|
6
|
4
|
2
|
6
|
RSC Anderlecht
|
3
|
0
|
1
|
2
|
2
|
6
|
-4
|
1
|
Galatasaray AŞ
|
3
|
0
|
1
|
2
|
2
|
9
|
-7
|
1
|
0 comments:
Post a Comment