Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Friday, October 24, 2014

NEWS:MAJAMBAZI WAIBA MABILIONI STANBIC BANK





Makao makuu ya Benki ya Stanbic yaliyopo Wilaya ya Kinondoni, barabara ya Alli Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.(picha kwa hisani ya mwananchi)
 Dar es Salaam. Watu 13 wakiwamo wafanyakazi tisa wa Benki ya Stanbic jijini Dar es salaam wanashikiliwa na polisi baada ya majambazi kuiba fedha zaidi ya Sh1 bilioni jana jioni.

Watu hao wanashikiliwa katika Kituo cha Oysterbay kwa uchunguzi zaidi wa uporaji huo uliofanywa na majambazi yenye silaha yaliyoingia katika Tawi la benki hiyo la Mayfair Plaza lililopo Barabara ya Mwai Kibaki na kutokomea na kitita hicho.

sample
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, amesema  kuwa watu wengine wanne wanaoshiliwa ni askari aliyekuwa lindo na wengine watatu ambao hakuwa tayari kuwataja.

Hata hivyo, chanzo chetu cha habari ambacho hakikutaka kitajwe gazetini, kilidai kuwa hadi jana alasiri, maofisa wa benki hiyo waliokuwa wanashiriki uchunguzi, walibainisha kuwa kiasi cha zaidi ya Sh1.0943 bilioni kilikuwa kimeibwa.

Habari zilizopatikana baadaye kutokana katika chanzo chetu, zilidai kuwa fedha zilizoibwa ni Euro 260,000 (Sh598 million), Dola za Marekani 175,000 (Sh280milioni), Sh216 milioni za Tanzania, na pauni 190 za Uingereza (Sh380,000).

0 comments: