Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akiwa na kocha mwenzake wa Crystal Palace Neil Warnock wakiteta baada ya mechi kuisha ambapo the blues waliibuka na ushindi wa bao (2_1). |
KOCHA
wa Chelsea Jose Mourinho anaamini kuwa kwa namna kikosi chake
kilivyoenea kila idara, basi kinaweza kutwaa kombe kwenye ligi ya nchi
yoyote ile duniani.
Chelsea imeifunga Crystal
Palace 2-1 kwenye dimba la Selhurst Park na kuendelea kutakata kileleni
huku ikianza kuaminika kuwa wanaweza wafikia rekodi ya Arsenal
waliomaliza msimu bila kufungwa miaka kumi iliyopita.
Pamoja
na hayo Jose Mourinho inabidi awe makini mno kwani kitendo cha kumaliza
Ligi Kuu mikono mitupu, basi itakuwa ni anguko kubwa kwake.
0 comments:
Post a Comment