Mara
nyingi tumezoea kuona list za wasanii wakubwa wakitajwa kuingiza pesa
nyingi zaidi Afrika, wiki hii imetoka list iliyoandikwa na eDaily kupitia ripota Brian Okoth ambayo imewataja wasanii watano kutoka Afrika wanaotajwa kuingiza pesa nyingi zaidi mwaka 2016.
Diamond Platnumz (Tsh. Bilioni 9,665,923,190.55)
Mtanzania Diamond Platnumz
huenda akawa msanii anayezungumzwa au kutajwa sana kwasasa barani
Afrika kutokana na headlines anazotengeneza kila siku, mikataba yake na
makampuni makubwa kwenye kazi zake pia inazidi kumuweka sehemu nzuri
kifedha.
Hakuna
shaka kwamba Diamond ni mmoja kati ya wasanii wanaoingiza pesa nyingi
kupitia muziki wao kwasasa, na hili litaondoa utata kuhusu kiasi cha
pesa alichotajwa kuwanacho staa huyu wa single ya Make Me Sing ambaye aliwahi kuzungumza na E!TV
Jumapili ya, June 26 mwaka huu na ikaelezwa kuwa anamiliki pesa
zinazozidi kiasi cha dola Milioni Nne za Marekani (Zaidi ya Bilioni 9 za
Tanzania).
Kiasi
hicho cha pesa hakijaja tu kama suprise kwa Diamond, ambaye anatajwa
kuwa ndiye msanii anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye show au event
yoyote anayotakiwa kuhudhuria nchini Tanzania na pengine Afrika
Mashariki kwasasa.
Pesa
nyingi zinaelezwa kuingia kupitia shows alizofanya ndani ya
Tanzania, East Africa na nje ya Afrika. Diamond Platnumz pia amekuwa
balozi wa makampuni mengi makubwa ya biashara ikiwemo Vodacom, Cocacola, DSTV, Uber Taxi na Red Gold.
Ziko
taarifa kuwa Diamond Platnumz huchaji si chini ya shilingi milioni 25
kwa show moja ya kawaida akiwa Tanzania, pia gharama hizo hufikia
shilingi milioni 50 na kuendelea akiitwa na kampuni ya biashara na kama
akiitwa nje ya Tanzania basi gharama zake huanzia shilingi milioni 200
na kuendelea.
Vyanzo
vingine vya mapato ni pamoja na mauzo ya miito ya simu ambayo inaelezwa
hakuna msanii yeyote Afrika Mashariki anayefikia mauzo yake kwenye
ukanda wa maziwa makuu, pia anamiliki akaunti ya Youtube ambayo ipo
kwenye list ya chaneli 10 zinazoangaliwa zaidi barani Afrika.
Hivi karibuni Diamond Platnumz
ameingia kwenye biashara za kununua nyumba za zamani na kuzifanyia
ukarabati ambapo huzipangisha, kitu kinachotajwa kumuingiza mkwanja
mrefu zaidi jijini Dar es salaam, mbali na kumiliki record lebel yake ya
Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo kwa mujibu wake Diamond aliwahi kusema wamesaini deal ya zaidi shilingi Bilioni 2 na lebel ya Universal Music Group ya Marekani ili kusambaza kazi za wasanii walioko chini yake ambao ni Rich Mavoko, Harmonize na Rayvany.
Wizkid (Tsh. Bilioni 25,676,809,453.47)
Kwa mujibu wa Infoguide Nigeria, mpaka kufikia December 2015 mwimbaji star Wizkid
alikuwa anakadiriwa kumiliki kiasi cha dola Milioni 11.5 ambazo mpaka
mwisho wa mwaka 2016 inaelezwa kuwa amefikisha dola Milioni 12.
Wizkid amekuwa na mikataba inayomuingizia pesa nyingi na makampuni kutoka Nigeria ikiwemo label yake ya Star boy Records aliyoianzisha mwaka 2010. Pia mwaka 2014 Wizzy alisaini deal ya kuwa balozi wa kampuni ya simu ya MTN ambao walimlipa zaidi ya shilingi milioni 300 na kampuni ya MTN rival Globacom ikapanda mara mbili ili kumtumia Wizkid kama balozi wao.
Deal hiyo ya miaka miwili inatajwa kumuingiza Wizkid zaidi ya shilingi milioni 900 kutoka kampuni ya Globacom
na mwaka 2015 wakati akifanya sherehe ya kutimiza miaka 25 Wizkid
alisaini upya mkataba wake na kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi.
Ukijumlisha
kiwango cha pesa anachoingiza kutoa kwenye shows anazofanya, mauzo ya
nyimbo zake, tuzo, zawadi pamoja na mikataba yake, inamuweka star huyo
kwenye list wasanii wanaoingiza pesa nyingi zaidi nchini Nigeria. Zipo taarifa kuwa ili kuweza kumualika Wizkid aje kufanya show ya kampuni itakubidi umlipe si chini ya shilingi milioni 60.
Kumbuka pia mwezi August, 2015, WizKid alitajwa kwenye jarida la Forbes kama miongoni mwa mastaa 14 wanaoitangaza Afrika.
Davido (Tsh. Bilioni 30,502,418,406.03)
Kwa
mujibu wa Nigerian Finder wameeleza kuwa Davido anamiliki utajiri
unaofikia dola milioni 14 ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 30 za
Kitanzania.
Pamoja na
kuzaliwa kwenye familia yenye uwezo mkubwa kifedha, hiyo haikumfanya
Davido kurelax badala yake alitumia nafasi yake kama msanii kujenga jina
lake na kufanya biashara inayomfanya kuingiza pesa nyingi kwenye
akaunti zake.
Mwaka 2012, Davido alisaini deal na kampuni ya MTN TV
kama balozi na akasaini deal nyingine na MTN Pulse kuwa muwakilishi wa
kampuni hizo kwa kitita cha zaidi ya shilingi milioni 207 za Kitanzania,
wakati huo huo mwaka 2014, Davido alilipwa zaidi ya shilingi milioni 341 kuwa balozi wa kampuni ya dawa za meno ya Close UP.
Pia Davido
na kaka yake Adewale Adeleke wanamikili lebel ya muziki iitwayo HKN
Music ambayo imekuwa ikiwaingiza pesa nyingi kupitia mauzo ya nyimbo za
wasanii waliosaini lebel, mauzo ya albam pamoja mikataba ya matangazo.
Akothee (Tsh. Bilioni 132,683,540,000.00)
Huenda
ikakushtua sana kutokana na jina la msanii huyu kutokua kubwa sana au
kutofahamika sana kwa watu wengi, Mwimbaji Akothee kutoka Kenya anatajwa
kuwa na utajiri unaofikia dola za Marekani milioni 61 ambazo ni zaidi
ya shilingi za Tanzania Bilioni 132.
Mapema
mwaka huu, mitandao ya habari za mastaa nchini Kenya iliripoti kuwa star
huyo wa single ya Give It To Me alikuwa anamiliki zaidi ya shilingi za
Tanzania Bilioni 8.
Akothee
amekuwa akijishughulisha na biashara pamoja na kilimo huku chanzo
kingine cha mapato kikitajwa kuwa ni fidia aliyolipwa kama talaka na
mwanaume wa kizungu aliyeachana naye miaka kadhaa iliyopita.
P-Square (Tsh. Bilioni 277,752,822,639.34)
Wakiwa ni
mastaa pekee kutoka Afrika kutajwa na jarida la Forbes mara mbili kwenye
list ya wasanii wanaolipwa pesa nyingi zaidi Afrika, kundi la PSquare
limeendelea kuweka rekodi ya kufanya shows za gharama kubwa kupita
wasanii wote Afrika, huku wakipata mialiko kutoka kwa Marais wa nchi
zaidi ya 5 na usisahau, mastaa hawa wanamiliki ndege binafsi.
Kwa mujibu
wa jarida la watu maarufu la Forbes, mapacha hao Peter na Paul Okoye
wanaounda kundia la P-Square wanamiliki utajiri wa zaidi ya dola za
Marekani milioni 130 zinazotokana na mikataba ya kibiashara na makampuni
mbalimbali, biashara za mafuta, mauzo ya muziki na shows wanazofanya.
0 comments:
Post a Comment