Mchezaji nyota wa
Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21
jela baada ya kupatikana na makosa ya kutumia ulaghai wakati wa ulipaji
ushuru, vyombo vya habari nchini Uhispania vinaripoti.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la BBC,Babake, Jorge Messi, pia amehukumiwa kufungwa jela kwa kuilaghai Uhispania €4.1m (£3.2m; $4.6m) kati ya 2007 na 2009.Wakati wa kesi, waendesha mashtaka walisema maeneo salama yenye kinga dhidi ya ushuru Belize na Uruguay yaliyumiwa kuficha mapato kutokana na uuzaji wa haki za picha za mchezaji huyo.
Lakini Messi amesema hakufahamu lolote kuhusu masuala yake ya kifedha.
0 comments:
Post a Comment