Habari hii imeripotiwa na BBC Swahili kuhusu jamii moja nchini Malawi ambayo haithamini ubikira wa watoto wao wa kike. BBC
Swahili wameripoti kuwa katika jamii hiyo wazazi wanamlipa mwanaume
kumbikiri binti yao punde tu anapopata hedhi yake ya kwanza.
Jamii hiyo
inaamini kwamba kuwa na binti ambaye ni bikira ni mkosi kwa jamii,
wazazi na jamii kwa ujumla katika maeneo mengi ya kusini mwa Malawi
wamekuwa wakishikilia tamaduni hii kwa miaka na miaka.
Wanaume
wanaowabikiri watoto wa kike huchaguliwa na wazazi kuwaondolea mikosi,
na huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa unyagoni kisha
kuwatembelea shangazi wake kabla ya kujulishwa kwa ‘fisi’.
Mafisi
hulipwa takriban dola 7 ambayo ni kama Tsh 15,324 kwa kila kitendo cha
ngono na hao mabinti ambao wengi huwa na kati ya umri wa miaka
11-14. Fisi mmoja katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva ameiambia BBC
kuwa hajui kwa kweli amewabikiri wasichana wangapi……
>>>”kwa
kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104, hiyo ndio tamaduni zetu
pia hapa mwanamke akifiwa lazima aje kwangu nimuondolee mkosi hata
kabla ya kuzikwa kwa mumewe’‘.
Aniva
ambaye ana umri wa takriban miaka 40 ana wanawake wawili na watoto 5,
anasema kuwa pale anaposhiriki ngono na watoto hao huwa anapewa muda wa
siku 3 hivi kumsafisha na kumuondolea mkosi.Kulingana na tamaduni zao,
ikiwa mwanamke au binti anakataa asibikiriwe huwa wanaamini kuwa jamaa
zao watafuatwa na mikosi na magonjwa.
SOURCE: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment