Je unamiliki paka?
Nchini Kenya, virusi hatari aina ya FIV, vinaavyofananana kabisa na virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi vimegunduliwa katika paka mmoja kupitia uchunguzi wa kimaabara.
Hii ni baada ya uchunguzi wa kina wa damu ya paka huyo kuthibitisha uwepo wa viini vinavyofanana kabisa na vile vinavyoathiri binaadamu.
Wafugaji wa paka na wanyama wa nyumbani wameonywa kuwapeleka wanyama wao kufanyiwa uchunguzi wa afya wanapowashuku wanyama wao wanaugua.
Virusi hivyo vinaitwa FIV (Feline Immunodefficiency Virus).
Ugonjwa huo sio mgeni katika wanyama.
Mwaka wa 1986 madaktari nchini Marekani waligundua virusi vilivyofanana kwa karibu na vile vinavyoambukiza binadamu vya HIV.
Lakini hii ndio mara ya kwanza kwa virusi hivyo kugunduliwa nchini Kenya.
Madaktari wa maabara ya Lancet mjini Nairobi Waligundua kuwa virusi hivyo vinasababisha ukosefu wa kinga mwilini na kudhoofisha afya ya wanyama hao wanaopendwa na kuishi majumbani.
Hata hivyo waliwahakikishia wafugaji wa paka kuwa hakuna ushuhuda wowowte wa maambukizi kutoka kwa paka hao kwenda kwa binadamu.
Daktari Dhaval Shah badala yake amewashauri wafugaji wa paka kuwafungia paka wao ndani ilikuwazuia wasijamiane na wale paka wanaorandaranda mitaani ambao huenda wameambukizwa ukimwi wa paka.
''kimsingi ugonjwa huu ni Ukimwi wa waka, japo inaambukizwa kupitia kwa mate na mkwaruzano haswa paka wanapopigana''
0 comments:
Post a Comment