Baada ya rapper wa kundi la Gangwe Mobb, Luteni Kalama kuoa
mwanamke mwingine na kumwacha mchumba wake aliyemvisha pete, Isabella
ameibuka na kudai kuwa ni yeye ndiye aliyemwacha baada ya kumuona ni
mwanaume asiye na future.
Luteni Kalama na mke wake anayedaiwa kuwa rafiki wa ex wake, Isabella“Mimi na Kalama tulikuwa tumeshaachana muda mrefu kwasababu nimeona ni mwanaume ambaye hana future hawazi chochote, kwahiyo nikaona kwanini nijipotezee muda. Mwanaume anaamka saa saba, kwahiyo nikaona niachane naye,” Isabela alimuambia mtangazaji wa Jembe FM, Natty E.
Isabella
“Lakini watu wameona ilivyotokea gazeti wanahisi labda Kalama aliniacha mimi kitu ambacho sio kweli, hana uwezo wa kuniacha, mimi ndio nilimuacha. Na nafikiri stress zake ndio zimemfanya aende akamuoe rafiki yangu sasa si ni uchizi. Halafu mwanamke unaoa unaenda kukaa kwa mwanamke tena, yeye si ndio anakuwa ameolewa, kwahiyo yeye ni mwanaume ambaye ni kilaza,” aliongeza Isabela.
0 comments:
Post a Comment