Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Monday, June 6, 2016

Harufu ya viatu vya MB Dog iliwahi kumfanya P-Funk amtimue studio

Madee amesema mtayarishaji mkongwe wa muziki Bongo, P-Funk Majani aliwahi kuwafukuza studio kwa sababu ya kunuka kwa viatu vya MB Dogg.
Madee2
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EATV, Madee alisema, “Tumeenda kwa mara ya kwanza nimempeleka Mb Dog, mi kipindi hicho nishafanya kazi yake Mola kwa hiyo P-funk ananielewa vizuri. Kufika getini katufungulia Kajala, sasa kipindi hicho Mb Dog bado yupo rafu sana havai vizuri, tumeingia studio lakini ratiba anaijua Majani kwamba leo hawa machizi wanafanya ngoma.”
“Mb Dog si kavua viatu bwana, ile harufu ambayo ilikuwa inatokea studio, Majani akamind bwana, akawaka utadhani kimetokea sijui kitu gani huwezi amini hatukurekodi siku hiyo, ilibidi Mb Dog atolewe nje tuanze kuoshana oshana miguu, lakini bado mchizi ikawa tayari kashajitoa kwenye mood hatujarekodi,” aliongeza.

0 comments: