Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Monday, May 30, 2016

Vitu 5 vilivyopigwa marufuku kwingine lakini kwa Tanzania ni ruksa.....ONA HAPA INASHANGAZA


feature_did_you_know_blankNimekusanya list ya vitu 5 ambavyo kwa nchi za wenzetu kama Marekani, Ujerumani, Hispania, Ufaransa na Bangladesh pamoja na sehemu nyingine duniani ni vitu ambavyo kisheria vimepigwa marufuku lakini kwa huku kwetu ni halali kabisa kutumika.
Hii hapa list ya vitu hivyo.
1. Baby Walker
baby_walker_small
Mwaka 2004 Canada ilipitisha sheria ya kukataza Baby walkers ndani ya nchi hiyo.. walidai kwamba mtoto akitumia baby walker inasababisha mtoto achelewe kutembea na pia kudumaza akili. Mtu yoyote atakayekutwa anamiliki au ananunua kifaa hicho faini ni dola 100,000 au kifungo cha miezi 6 jela.
2. Tomato Sauce #HeinzKetchup
Heinz Tomato Ketchup
Kama ulihisi Tomato Sauce zote ni ruksa kila sehemu basi jibu ni hapana. Mwaka 2011 tomato sauce ya ‘HEINZ TOMATO KETCHUP’ ilikatazwa kutumika kwenye Kanteen za shule Ufaransa na pia ilikatazwa kusafirishwa kwa baadhi ya nchi za Ulaya.
3. Mifuko ya Rambo.
Groceries are carried in plastic bags in San Diego, California September 30, 2014. Single-use plastic bags are set to disappear from California grocery stores over the next two years under a first-in-the-nation state law signed on Tuesday by Democratic Governor Jerry Brown, despite opposition from bag manufacturers.      REUTERS/Mike Blake (UNITED STATES - Tags: ENVIRONMENT BUSINESS) - RTR48EFU
Nchi ya kwanza kukataza mifuko ya rambo kutumika ni Bangladesh kwa sheria iliyopitishwa huko mwaka 2002.. California nako walipitisha Sheria hiyo mwaka 2012-13 na mpaka sasa hakuna sehemu utaenda California alafu ukawekewa kitu kwenye mfuko wa rambo.
4. Big g
getty_rf_photo_of_chewing_gum_in_wrapper
Mwaka 1992 Singapore ilipitisha sheria iliyokataza kuuza ama kusafirisha big g kwa nchi yoyote duniani, ila big g zitengenezwe kwa ajili ya kulika na kununuliwa na raia wa Singapore tu. Baada ya miaka 12 yalifanyika mabadiliko na kuruhusu watu wa Singapore kununua big g ambazo hazina sukari yani Sugar-free chewing gums ambazo ni nzuri kwa meno na kinywa cha binadamu. Kwa sasa utaratibu uliopo ukikutwa unatema big g chini au unatafuna ovyo unapigwa faini.
5. Majina ya watoto
tea-collection-3.2 
Ujerumani na Denmark kisheria hawaruhusiwi kuwapa watoto majina yoyote nje ya majina 7000 ambayo tayari yamepitishwa, ikitokea mtu atapenda kumuita mwanae jina alipendalo basi atatakiwa kuomba kibali maalum kanisani alafu baadae maombi hayo yanawasilishwa Serikalini, jina likipitishwa basi unaruhusiwa kulitumia

0 comments: