Mkuu
wa zamani wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na mshauri wa Rais wa Zanzibar
kisiwani humo, Dadi Faki Dadi amekamatwa akituhumiwa kufanya mapenzi na
mtoto wake wa kambo.
Dadi
alikamatwa juzi akidaiwa kukutwa na mtoto huyo wa mkewe wa ndoa mwenye
umri wa miaka 21 katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa Executive,
jirani na makao makuu ya Uhamiaji Zanzibar katika eneo la Kilimani chini
na Maisara, mjini Unguja.
Mwanasiasa
huyo alijikuta akipigwa pingu na polisi akiwa kifua wazi mbele ya mkewe
na wanafamilia na kisha kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi
Mwembemadema.
Picha
za video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zilimwonyesha Dadi
akikabiliwa na mashambulizi makali ya maneno kutoka kwa watu
waliomkamata, akiwamo mkewe.
“Mwacheni avae nguo kwanza, mpeleke bwana, twende bwana..." ni baadhi ya maneno yanayosikika katika video iliyorekodiwa wakati wa kumtia mbaroni.
Taarifa
zilizopatikana miongoni mwa wanafamilia ya kiongozi huyo, zilidai
kwamba alikamatwa baada ya kumtilia shaka binti huyo kutokana na
mienendo yake ya hivi karibuni na kuamua kumfuatilia.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha
kumshikilia Dadi kwa muda kabla ya kumwachia kwa dhamana.
“Kijamii
alitenda kosa, lakini sisi tunaendelea kufanya uchunguzi, iwapo
tutabaini ametenda kosa la kisheria na anaweza kuwa mashtaka tutamkamata
ili kumpeleka katika vyombo vya sheria,” alisema Mkadam.
Mmoja wa wanafamilia ambaye aliomba jina lake lisitajwe alisema: “Mwizi siku zake ni arobaini, tulimtega na hatimaye tumemnasa sasa tuone mwisho wake utakuwa nini na kipi kitajiri baadaye.”
ANGALIA VIDEO YA FUMANIZI HAPA
0 comments:
Post a Comment