Kesi
iliyokuwa inamkabili staa kutoka Marekani Chriss Brown juu ya malezi
mabovu ya mtoto wake ambayo ilifunguliwa na mzazi mwenzake Nia Guzman,
May 24 maamuzi yalitolewa na Mahakama ya Califonia.
Mama mtoto
wa Royalty alidai kuwa Chris hana malezi sahihi na muongozo unaostahili
juu ya mtoto wao, amesema Chris amekuwa akivuta sigara na bangi yeye na
marafiki zake mbele ya mtoto wao na imempelekea Royalty kupata maradhi
ya pumu.
Nia Guzman
aliomba mahakama impunguzie Chris muda wa malezi ya mtoto huyo na
kuomba yeye ndiye achukue jukumu la usimamizi wa mtoto wao kwa kipindi
hiki. Chriss Brown ameshinda kesi hiyo ambapo maamuzi ya jaji yaliruhusu
malezi sawa kutoka kwa wawili hao ambapo Chriss anaruhusiwa kuspend
siku 12 na mtoto wake kila mwezi bila masharti yoyote.
Hata hivyo
Nia Gozman alidai kuongezewa fedha za malezi ya mtoto kutoka USD2500
ambazo ni kama milioni 5 za kibongo mpaka USD16000 sawa na milioni 35
kwa mwezi kitu ambacho Chris alisema mzazi mwenzie anamtumia mtoto
kupata pesa za kujikimu binafsi.
0 comments:
Post a Comment