Wema Isaac Sepetu ‘Madam’
STORI: Mwandishi Wetu, Ijumaa
Dar es Salaam: Endapo mkali wa sinema za
Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ atalivalia njuga suala la
kudhalilishwa mtandaoni na msanii aliye chini ya Lebo ya Wasafi Classic
Baby (WCB), Rajab Abdulhan ‘Harmonize’, jamaa huyo atakwenda jela miaka
kadhaa na faini juu.
CHANZO NI NINI?
Juzikati, Harmonize au Hamo, akiwa na
kundi la wasanii wenzake katika eneo ambalo halikujulikana ni wapi,
walijichukua clip (kipande cha video) kwa staili ya kujipiga ‘selfie’
huku Harmonize akiimba wimbo wa msanii Stamina uitwao Mwambie Mwenzio,
ambao kwenye mistari hiyo dogo huyo alisherehesha kwa kusema kuwa,
usitoe mimba usije ukaja kulia kama (Wema) Sepetu.
HARMONIZE ALA ZA USO
Baada ya Harmonize kuwaongoza vijana hao
kumdhalilisha Wema kwa staili hiyo, watu wengi kupitia mitandao
mbalimbali ya kijamii walimpa jamaa huyo za uso, baadhi wakisema kuwa,
umaarufu mdogo alioupata unamzuzua.
“Huyu mtoto anaona ameshakuwa maarufu
sasa, anaona sawa kuwatukana hata wakubwa zake au ametumwa?” alihoji
mmoja wa mashabiki wa Wema (Team Wema) aliyejitambulisha kwa jina la C_K
kwenye Mtandao wa Instagram.
Mwingine akaandika: “Ninachojua huyu
dogo anatafuta kiki lakini siyo kwa kufanya mambo haya, hivi ana
ushahidi gani kama Wema katoa mimba?”
KAULI YA TCRA
Akizungumzia sakata hilo, Afisa kutoka
Dawati la Malalamiko wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Doris
Mhimbira alisema kuwa ni kosa la jinai ambalo mlalamikaji akiwa
‘serious’ anaweza kusababisha Harmonize akachukuliwa hatua kali za
kisheria.
Alisema kitendo alichokifanya Harmonize,
endapo Wema atakwenda kulalamika na uzuri ni kwamba jina la mlalamikiwa
linajulikana hivyo sheria itachukua mkondo wake. (Kwa mujibu wa sheria
ya mtandao anaweza kwenda jela kati ya mwaka mmoja hadi saba na faini
juu.)
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana ni
kwamba Wema hajalikalia kimya suala hilo kwani anadaiwa kawasiliana na
wanasheria wake ili kumfunga jamaa huyo.
MAMA WEMA SASA
Hata hivyo, wakati kila kona yakirushwa
makombora kuelekezwa kwa Harmonize na timu yake (Team Harmonize),
yakavuja madai kuwa, mama wa Wema, Mariam Sepetu aliona clip hiyo na
kwamba alikwenda kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini) ili
kushinikiza kijana huyo kukamatwa na sheria ichukue mkondo wake.
WEMA AJIBU KIAINA
Baada ya Wema kuona clip hiyo alionekana
kuumizwa na maneno hayo, akaamua kutupia picha mtandaoni akiwa na mama
yake kisha akaandika; ‘Ipo siku na mimi nitaitwa mama’.
HARMONIZE ATAFUTWA!
Kufuatia ishu hiyo kuwa gumzo mjini huku
kila mmoja akimlaumu Harmonize, Ijumaa lilimtafuta kupitia simu yake ya
mkononi ambapo alipopatikana alisema, anashangaa watu kumjia juu kwa
kuwa yeye hakumtaja Wema kwenye clip hiyo ila jina lililotajwa ni
Sepetu.
“Tuachane na hayo mambo bwana, mimi
sijamtaja Wema pale, jina lililotajwa ni Sepetu sasa Wema na Sepetu wapi
na wapi?” alijitetea Harmonize.
SEPETU GANI?
Alipobanwa kuwa ni Sepetu gani ambaye walikuwa wakimlenga ambaye ametoa mimba, hakujibu badala yake alikata mawasiliano.
IJUMAA LAMTAFUTA MAMA WEMA
Mwandishi wetu alifanya jitihada za
kumtafuta mama Wema ili kujua aliichukuliaje clip hiyo na kama ni kweli
alikwenda polisi, hata hivyo simu yake iliita kwa muda mrefu bila
kupokelewa.
WEMA HUYU HAPA
Baada ya mama Wema kukosekana, Ijumaa
lilipata fursa ya kuwasiliana na Wema ambaye katika hali ya kuonesha
kutofurahishwa na kitendo hicho, alimbutua Harmonize kwa kusema kuwa
hajitambui ndiyo maana anafanya mambo ya kitoto.
“Kwanza nipo bize sana na kazi, hao ni watoto wadogo hao hawajielewi,” alisema Wema.
Alipoulizwa kwamba huenda ni mpango wa
kumtibulia mchongo wake anaoupigia kampeni wa Wema App, mwanadada huyo
alisema kama ni hivyo yeye na walio nyuma yake siyo wasomi na bora
kuachana nao.
Hata hivyo, taarifa zilizovunjwa ni
kwamba, Harmonize anafanya kila awezalo ili kumpa mimba mpenzi wake wa
sasa, mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe.
Harmonize alipoulizwa kuhusu hilo alisema kuwa, hiyo ni mipango ya Mungu na ikitokea itakuwa mwake tu.
TUJIKUMBUSHE
Katika mambo ambayo yamekuwa yakimuumiza
Wema ni pamoja na watu kumuita mgumba sambamba na kumpa skendo ya kutoa
mimba kila anaponasa.
Katika siku za hivi karibuni, Wema
alinasa mimba lakini inavyonekana haikuwa riziki kwani miezi kadhaa
baadaye ilidaiwa kuchopoka.
SOURCE:GPL
0 comments:
Post a Comment