POLISI mkoani Singida inamshikilia Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Itaja na mkewe kwa tuhuma za kumfungia ndani ya chumba mtoto wao mlemavu wa viungo kwa miaka 12 bila kutoka nje.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka aliwataja watuhumiwa hao
kuwa ni David Mtipa (59) ambaye ni Mchungaji wa Kanisa hilo na mkewe
Mariam Philipo (45) wote wakazi wa kijiji cha Itaja katika tarafa ya
Mgori wilayani Singida.
Kamanda
Sedoyeka alisema tukio hilo liligundulika juzi katika kijiji hicho
baada ya Polisi kupata taarifa za siri kutoka kwa wasamaria.
Akielezea tukio hilo, Kamanda Sedoyeka alisema watuhumiwa walimfungia ndani ya chumba mtoto huyo, Timotheo David (30) kwa muda wa miaka 12 huku huduma zote za kibinadamu, ikiwemo haja ndogo na kubwa pamoja na chakula zikifanyika humo ndani.
Akielezea tukio hilo, Kamanda Sedoyeka alisema watuhumiwa walimfungia ndani ya chumba mtoto huyo, Timotheo David (30) kwa muda wa miaka 12 huku huduma zote za kibinadamu, ikiwemo haja ndogo na kubwa pamoja na chakula zikifanyika humo ndani.
“Baada
ya timu ya askari wa Upelelezi na Ofisa Ustawi wa Jamii kufika eneo
hilo wakiwa na viongozi wa kijiji na kufanya mahojiano, watuhumiwa
walikiri kumfungia chumbani mtoto wao huyo na kwamba ni mlemavu wa miguu
na mikono, lakini pia ni mlemavu wa akili,” alisema Kamanda Sedoyeka na kuongeza:
“Wamesema
mtoto wao alizaliwa mwaka 1984 akiwa mzima, lakini alipofika darasa la
sita 2003 alianza kuugua ugonjwa usiojulikana ikiwa ni pamoja na
kuanguka kisha kutoa povu mdomoni huku mwili wake ukibadilika rangi kuwa
ya njano na kutibiwa bila mafanikio.”
Aidha,
alisema mlemavu huyo alitibiwa maeneo mbalimbali bila mafanikio na
ndipo wazazi hao walipoamua kumfungia ndani baada ya kuona
wanafedheheshwa mbele ya jamii huku akila chakula, kujisaidia humo
chumbani na kutoruhusiwa kutoka nje.
Kutokana
na hali hiyo, majirani waliingiwa na hofu kwa kutomwona mtoto huyo kwa
kipindi kirefu kiasi hicho hali iliyozua maswali mengi.
Wakati baadhi walijua huenda ameuawa, wengine walihusisha kitendo hicho na imani za kishirikina huku Mchungaji akidaiwa kuzidiwa maarifa na mkewe.
Wakati baadhi walijua huenda ameuawa, wengine walihusisha kitendo hicho na imani za kishirikina huku Mchungaji akidaiwa kuzidiwa maarifa na mkewe.
Alisema
kitendo cha kumfungia mtoto huyo ndani kwa kipindi chote hicho,
kumwacha akiwa uchi na kumlaza kwenye kitanda cha kamba kisichokuwa na
godoro ilikuwa ni ukiukwaji wa misingi ya binadamu na si cha kiutu.
Alisema
amepelekwa Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa matibabu na uchunguzi zaidi
wa afya yake wakati wazazi hao wakishikiliwa na kuhojiwa ili hatimaye
wafikishwe mahakamani kwa ukatili uliovuka mipaka.
0 comments:
Post a Comment