Kilichojificha nyuma ya pazia la uhusiano wa mastaa wa Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, na Shamsa Ford sasa kimevuja baada ya mtandao huu kunasa habari za wawili hao kuwa kwenye uhusiano wa mapenzi kiasi cha kudaiwa kupika na kupakua pamoja.
Chanzo kimeeleza kwamba, wawili hao ambao kila mmoja katika
siku za hivi karibuni aligombana na mwenza wake wa awali, wamekuwa
katika uhusiano wa kimapenzi kwa uficho wa hali ya juu, wakionekana mara
kwa mara nyumbani kwa Mbongo Fleva anayeishi Kimara Korogwe, jijini
Dar.
Inadaiwa kuwa kwa zaidi ya wiki tatu sasa wawili hao wamekuwa
wakionekana katika gari moja, wakitoka au kuingia nyumbani kwa Nay
wakitokea mjini kwenye mihangaiko yao ya kila siku.
“Kama ulikuwa hujui vizuri naomba nikujuze, Nay na Shamsa wanaonekana
walikuwa wakifuatiliana kwa muda mrefu, nasema hivi kwa vile siku
chache tu baada ya wawili hawa kuachana na watu wao wa zamani, leo wako
pamoja tena wanaonyeshana mahaba utadhani walikuwa pamoja miaka mia
iliyopita,” alisema mtoa habari wetu.
Ili kuthibitisha maneno yake, chanzo chetu kilituma picha kadhaa za
wawili hao wakiwa nyumbani kwa Nay, huku akisisitiza kuwa hata dada na
ndugu wa mwanaume huyo, nao wamekuwa wakipost picha za Shamsa ambaye
hivi sasa anapika na kupakua nyumbani kwa mkali huyo wa kibao cha Nakula
Ujana.
Nay wa Mitego alipoulizwa kuhusu ukaribu huo,
alisema hadhani kama ni jambo la haki kwake kuulizwa kuhusu suala hilo,
wakati inajulikana kuwa yupo ‘single’.
0 comments:
Post a Comment