Imelda mtema
MAUZAUZA! Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’ amepatwa na dhahama ya aina yake baada ya kuibiwa nguo yake ya ndani kimazingara kisha kuikuta nje ikiwa imeloa damu, Ijumaa lina mchapo kamili.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mara nyingi Kajala ana kawaida ya kufua na kuzianika nguo hizo ndani lakini katika mazingira ya kutatanisha moja ilipotea na kila alipofanya jitihada za kuitafuta, hakuiona.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, baada ya nguo hiyo kutooneka ghafla, Kajala alichanganyikiwa sababu nyumbani kwake hakuna hata panya ambaye anaweza kuibeba pengine na kuitupa sehemu nyingine.
Chanzo hicho ambacho kipo karibu sana na Kajala kilizidi kutiririka kuwa, baada ya kulitafuta ‘kufuri’ hilo kwa muda mrefu bila mafanikio, alikuja kulikuta kwenye ndoo tupu ya maji tena ikiwa imetobolewa huku ikiwa imetapakaa damu.
“Baada ya Kajala kuona hivyo alipandwa na presha kwa kuwa hakutegemea kuiona ikiwa katika hali kama hiyo,” kilidai chanzo hicho.Baada ya chanzo hicho kuweka nukta, Ijumaa lilimvutia waya Kajala ili kuweza kupata undani zaidi wa tukio hilo:
Ijumaa: Pole Kajala na mkasa uliokupata.
Kajala: Mkasa gani tena jamani.Ijumaa: Si wa kuibiwa nguo yako ya ndani na kuikuta imetobolewa huku ikiwa na damu!Kajala(Mshangao) hiyo habari mmeipata wapi nyie kweli dunia haina siri, yeah! Ni kweli ilitokea lakini sitaki kuizungumzia sana hivi vitu si vya kuanika kila mtu ajue, nashukuru Mungu kwa kunipigania.
0 comments:
Post a Comment