Taarifa KUTOKA Wilayani Rungwe, Jijini Mbeya inaeleza kuwa Basi dogo aina ya Toyota Hiace imetumbukia kwenye Mto Kiwira mapema leo na inadaiwa kuwa zaidi ya watu 18 waliokuwepo kwenye basi hilo wamepoteza Maisha.
wa mujibu wa mtoa taarifa, amesema kwamba ajali hii imetokea wakati Mabasi yafanyayo safari zake kati ya Mbeya na Kyela (maarufu kama Coaster) kugoma kutoa huduma ya kusafirisha abiria katika maeneo hayo, hivyo baadhi ya hiace za mjini kuamua kubeba abiria, hali iliyopelekea hiace hizo kubeba abiria wengi zaidi ya uwezo wake.
Inaelezwa kuwa gari hiyo ilipoteza muelekea na kuingia mtoni, baada ya dereva wake kushindwa maarifa kutokana na mwendo aliokuwa nao.
Mungu aziweke pema roho za marehemu hao,Amin.
Pichani ni Baadhi ya wakazi wa maeneo ya jirani na ilipotokea ajali hiyo wakiiangalia basi hiyo ikiwa kando kando ya mto Kiwira.
Wananchi wa Mji wa Kiwira wakienda kuangalia ajali hiyo.
Sehemu ya wananchi wa Mji wa Kiwira wakiangalia Baadhi ya Miili ya Watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Imetokea
katika mto kiwira Tukuyu Wilayani Rungwe mkoani Mbeya
0 comments:
Post a Comment