Watu wengi tumewaona kwenye ndoa wakiishi katika hali tofauti za maisha, wako wenye fedha na wasionazo, wako wenye furaha na wasio na wasionao. Yote hii huweza kuchangiwa na sababu nyingi ikiwemo wanandoa hawa kujikuta wanaingia katika ndoa wakisukumwa na sababu zilizo mbovu na zisizo na msingi.
Ziko sababu njema na nzuri za ndoa
zinazoongelewa sana na wengi maeneo mbalimbali.
Mimi nimejaribu kuzitafuta zile sababu zisizo nzuri ambazo wengine
pasipokuwa makini wamezishikilia na kusiruhusu sababu hizi ziwasindikize katika
ndoa na hivyo kujikuta wenajuta na kulia katika muda mwingi wa
maisha.
Hii pia ni sababu ya ukweli kwamba
siku hizi idadi ya ndoa zinazovunjika ni kubwa sana kuliko zamani. Hali ya kiwango cha kudhamiria (commitment)
kwa wanandoa ni kidogo sana na hivyo kushusha uthamani wa ndoa
zenyewe.
Sababu hizi zitakuwezesha kuubadili
mtazamo ulionao juu ya ndoa na kukupelekea kubadili namna unavyo sema au kuwaza au kutenda kuhusiana na
suala zima la ndoa.
SABABU MBOVU
- Kuingia katika ndoa kwa lengo la kusaidiwa au kuongeza kiwango cha kiuchumi ulicho nacho.
hapa wengine wamewageuza wapenzi wao
kuwa mitaji au rasilimali ya kuwaondoa wao pamoja na ndugu zao kutoka kwenye
umasikini. Kwa kuthibitisha hili
wengine wamepewa majina kama BUZI, ATM n.k.
Katika penzi la namna hii hakuna
mguso au muunganiko wa kuhisia baina ya wapenzi, bali kinachowaunganisha pekee
ni kile kilicho mfukoni. Athari za penzi la aina hii lina fungua milango mingi
kwa wanandoa kutokuwa waaminifu na hata kujihusisha na mapenzi
nje ya ndoa.
- Hofu ya umri kupita na kuzeeka
Wako wengi sana, hususani watu wa
wajinsia ya kike ambao wamejikuta wakiwakubali wanaume wa aina yoyote ili mradi
tu nao waolewe maana umri wao ulionekana kusonga sana na hofu ya kutoolewa
kutanda.
Mwanaume anayehusiana na mwanamke
mwenye tabia hii huulizwa au kulazimishwa kila siku kwenda kujitambulisha kwa
wazazi wa binti au kutangaza ndoa. Ndoa
nyingi za aina hii zimeishia kenye talaka na kutengana.
Wako wengine ambao, kwasababu
wanakiu sana ya kupata watoto na wameogopeshwa sana habari kwamba wana weza
wasipate watoto kwa sababu ya umri wao, basi watacheka na kaka yeyote yule ilimradi tu waolewe au
wazae naye Wengine wajinsi hii wamejuta
sana baada ya kujikuta kuwa waliyezaa naye hakuwa BABA wa kweli bali kirukanjia tu na
kwahiyo wameishia kulea mtoto au watoto wao wenyewe pasipo mzazi wa pili, jambo
ambalo kwa kiasi kikubwa linawaathiri
watoto wengi. Kwa wale wanaokimbilia
kuolewa ili wakazae watoto, kukumbuka kuwa hata huko kwenye ndoa kuna waliokosa
watoto.
- Kuingia kwenye ndoa sababu ya mimba au mtoto aliyepatikana kabla ndoa
Lazima kutofautisha kuwa sababu
iliyowapelekea kuzaa mtoto siyo itakayowapelekea kuoana. Acha sababu ya kuoana kwenu iwe penzi lenu la
dhati na sio mimba au mtoto.
Suala hili linahitaji pia wazazi
wajue kwamba kitendo cha watoto kupeana
mimba au kupata mtoto hakitoshi kuwa sababu ya kuwalazimisha kuoana, maranyingi
wazazi wamewalazimisha watoto wao kuingia katika ndoa sababu ya mimba au mtoto
na kujikuta wanawaharibia maisha yao mazima.
- Kulazimika kuingia kwenye ndoa au mahusiano ya kudumu kwasababu ya upweke, (Loneliness). Mara nyingi mtu anapokuwa peke yake (single) huwaza kuwa ndoa ndiyo inayoweza kuwa utatuzi mkubwa wa matatizo yake. Nakubaliana na ukweli wa maandiko kwamba “Sio vema mtu awe peke yake…” lakini ni vizuri tukijua tofauti iliyopo baina ya kuwa peke yako na upweke. Hivi ni vitu tofauti: kuwa peke yako inamaanisha kukosa mawasiliano au ukaribu na watu wengine, unakuwa kama uliyetengwa, wakati upweke (loneliness) inahusisha nafsi, akili na hisia kuwa pweke au kujihisi kutengwa na hii ni ngumu kuishuhulikia. Ni heri kuwa peke yako (single) kuliko kuwa kwenye ndoa na bado ukajisikia upweke (lonely). Wako wengine waliodhani ndoa ni suluhisho la upweke waliokuwa nao na mara walipoolewa au kuoa, mawasiliano baina yao yakayumba na hivyo kukomaza upweke kwa wote wawili.
- Kuolewa au kuoa kwasababu ya shinikizo kutoka kwa wazazi,ndugu au marafiki
Shinikizo hizi zaweza kuwa za
kihisia au hata kihalisia. Kihisia ni
pale ndugu au wazazi wanapokushawishi mara kwa mara kuoa sababu umri wako una
pita na wako wazazi wengine husema wanataka wajukuu. Hata kama huhisi kulazimishwa lakini kwa kule kurudia rudia
kwa kukumbushwa kila siku kunaathiri hisia zako na kuweza kukupelekea kuingia
katika ndoa isiyopangiliwa. Shinikizo ya
kimwili au kihalisia ni pale wazazi wanopolazimisha watoto wao kuoa au kuolewa
na watu fulani kwa sababu tu ni marafiki zao (family friends) au kwa sababu ya
kulinda utajiri na matarajio yoyote binafsi.
Ndoa nyingi za aina hii zimekuwa kero na dimbwi la maumivu na machozi,
baada ya muda kidogo mna jikuta mali mnazo, wazazi wenu wanapatana, lakini nyie kama wapenzi ni maadui
wakubwa.
- Kuamua kuoa au kuolewa ili kupata Uhuru.
Hii hutokea sana kwa wale waliozoea
kubanwa sana na wazazi katika kila wafanyacho hususani katika maamuzi. Wengine huzikimbia familia zao maana
hazieleweki, hazina mpangilio na hivyo kutamani kutoka ili wakaanzishe zakwao
wenyewe. Kinadada na kinakaka wanachoka kuamuliwa na kuwekewa masharti ya kuvaa,
kula, kufanya mambo, kutoka na kurudi kwa muda kwahiyo wanadhani ndoa ndio
itawachomoa kifungoni hapo.
MATOKEO YA KUINGIA KATIKA NDOA KWA
SABABU MBOVU
Lengo la kuingia kwenye ndoa, liwe
zuri au liwe baya ndilo litakalotegemeza aina ya maisha yenu katika ndoa hiyo
kuwa ya furaha au ya machungu. Baada tu
ya kuoana na huyo mtu wako kwa sababu zisizo za msingi, siku, miezi au miaka
siyo mingi utaanza kuchoka na kutamani kutoka nje ya hiyo ndoa kwamaana baina
yenu hakuna muunganiko wa kindani ya ndoa ya jinsi hii. Na mara nyingi hali hii hupelekea msongo wa
mawazo, mfadhaiko na kukosa furaha ndani ya ndoa. Na matokeo ya hali hii kumfanya mwanandoa
mmoja au wote wawili kuanza kutafuta kutoshelezwa na kuliwazwa nje ya ndoa na
hapa vinazaliwa vitu kama uzinzi, kutengana na talaka.
Kwanini Ndoa nyingi
hushindwa:
Kwa sababu ya kukosa maarifa.
Wanandoa wengi
hawajui nini wafanye, nini waelewe ili
kufanya ndoa yao zifanikiwe. Thamani ya
ndoa na jinsi ndoa inavyochukuliwa
sikuhizi ni tofauti sana na nyakati za wazazi wetu, na hii imewafanya wengine
kujikuta wako wenye ndoa kwasababu mbovu na hivyo ndoa nyingi kuvunjika au
kuyumba baada ya muda mfupi tu. Vitu kama kudhamiria, heshima na uaminifu sio
vya maana tena siku hizi, sababu watu wanaogopa kuonekana wazamani na
washamba.
Mtazamo wa ulimengu juu ya ndoa
umeharibiwa na magazeti, luninga na vitabu mbali mbali. Siku hizi kuishi bila ndoa ni kitu cha
kawaida, kuwa na mpenzi nje ya ndoa sio kitu cha kutisha tena, mapenzi nje ya ndoa sio ya kushangaza hata
kidogo. Kinyume chake ukionekana
kuyashangaa haya, jamii itakushangaa wewe kwa jinsi ulivyo nyuma ya wakati. Mambo yamebadilika sana, zamani binti
akikutwa bikira wakati anaolewa ilikuwa sifa kwake na familia nzima, siku hizi
binti akikutwa bikira atachekwa, na watu kumshangaa wakihisi ana matatizo
fulani. Hali kadhalika kwa kijana wa kiume aliyejitunza. Kwa bahati mbaya
sana tunaishi katika jamii ya ajabu
isiyoamini katika kujitoa kwa kweli na kudhamiria katika ndoa. Jamii isiyoamini
katika uaminifu, na ndiyo maana magomvi mengi hutokea pale simu ya mmoja
inapoguswa. Kuwindana na kuchunguzana
kumekuwa kawaida, maadili sio jambo la kuzingatiwa tena. Wanandoa wengi ni wale wenye majeraha ya
moyoni na walio umizwa, kwa hiyo hutoka nje ya ndoa zao wakitafutatafuta
mwingine aliyeumizwa kama wao ili
waliwazane.
Kwa haraka tuangalie sababu za
msingi zinazoweza kukufanya uingie katika ndoa na usijute.
-
Ndoa ni mpango
wa Mungu kwa mwanamke na mwanaume kuwa pamoja
-
Ni nafasi ya
wawili hawa kuonyeshana mapenzi
yao
-
Ni nafasi ya
kutimiziana mahitaji ya mwili kupitia tendo la ndoa kwa muda sahihi, na kwa mtu
sahihi, maadili yakizigatiwa.
-
Hamu na kiu ya
kutengeneza famila yenu.
-
Kutimiza kiu ya
kuwa pamoja kwa umoja (companionship)
-
Nia au kusudi la
kushiriki vyote kwa pamoja . Kufanya kutenda kwa pamoja ili kutimiza mahitaji
yetu wote.
-
Nafasi ya kutumia kwa manufaa kila uwezo na vipawa mlivyokuwa
navyo.
-
Kuchangiana
katika makuzi yenu ya ujumla, makuzi ya kimwili, kiriho, kihisia n.k
0 comments:
Post a Comment