Katika Mataifa yenye utamaduni wa kuongozwa na familia za kifalme au malkia Utawala wa Malkia Elizabeth wa Uingereza ndio maarufu kuliko familia zote zinazoongoza.
Japo familia hii ni maarufu lakini sio
tajiri kama ambavyo watu wanaweza kudhani wakilinganisha umaarufu na
ukubwa wa nchi anayoiongoza, Malkia Elizabeth na uwezo wa kifedha.
1:Familia ya kifalme inayoongoza taifa la Lichtenstein ndio inayoongoza kwa utajiri ikiwa na utajiri wa paundi bilioni 4.9.
Ikiongozwa na Prince Hans-Adam II,
familia hii ina utajiri ambao hauna uhusiano wowote na kodi za wananchi
wa taifa dogo la Lichtenstein na utajiri walio nao kina Hans-Adam II unatokana na kampuni ya LGT Holdings
ambayo inajiendesha kwa faida kubwa tofauti na familia nyingine za
kifalme ambazo zina utajiri unaotokana kwa kiasi kubwa na kodi za
wananchi wao.
2:Familia ya Kifalme ya Monaco inayoongozwa na Prince Albert II
inashika nafasi ya pili kwa wafalme na Malkia wa Ulaya ambapo ina
utajiri wa paundi bilioni 1 wakiwa wanaendesha biashara ya makazi kwenye
eneo la Monaco ambalo ni moja ya mataifa madogo kuliko yote duniani.
3:Familia ya Malkia Elizabeth ambayo inafahamika kama familia ya Windsors
yenyewe ina utajiri wa paundi milioni 295 ikiwa inaongoza mataifa ya
Uingereza na visiwa vyake vinne, Canada, Australia, New Zealand na
maeneo mengine ya Jumuiya ya Madola.
4:Familia ya kifalme ya Uholanzi inayofahamika kama Orange-Nassau
inashika nafasi ya nne kwenye orodha ya familia za kifalme zenye
utajiri . Familia hii ina utajiri unaokadiriwa kufikia paundi milioni
131 ambao kwa kiasi kikubwa unatokana na biashara binafsi zikiwemo
kampuni ya mafuta ya Shell.
Utajiri wa familia hii ya kfialme ya
Uholanzi unadhaniwa kuwa mkubwa zaidi ya makadirio haya kutokana na
ukweli kuwa haujawahi kutamka wazi kiasi cha fedha kinachomilikiwa na
familia hii.
5:Familia ya Bernadotte ya Sweden ambayo inaongozwa na Mfalme Carl Gustaf XVI inashika nafasi ya tano nyuma ya familia inayoongoza Uholanzi.
Familia
ya kifalme ya Hispania ni moja kati ya familia zenye utajiri mdogo japo
inamiliki kasri kubwa kuliko zote za kifalme duniani.
Familia hii inautajiri wa paundi milioni 27.5
Mfalme wa Norway, Harald V ndiye kiongozi mwenye utajiri kiduchu kuliko wote akiwa na kiasi cha Paundi milioni 12 pekee.
0 comments:
Post a Comment