Bi.Valerie Amos mkuu wa kitengo cha misaada wa umoja wa Mataifa |
Mkuu
wa kitengo cha misaada cha Umoja wa Mataifa Valerie Amos ,amesema
kwamba hali ya sasa nchini Syria ni doa katika jamii ya
kimataifa,ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mkakati mkubwa wa misaada
ya kibinadamu kuwahi kutokea.
Bi Valie Amos amesema kwamba zaidi ya dola milioni kumi na sita zinahitajika kusaidia harakati za Umoja wa mataifa duniani kwa mwaka ujao,na nusu ya fedha hiyo inahitajika nchini Syria pekee.
Umoja huo umesema kwamba wa Syria wapatao milioni tatu wameikimbia nchi yao kufuatia mapigano yanayoendelea na kukimbilia nchi jirani na wengine milioni kumi na mbili wenye uhitaji wakiwa wametawanyika nchini humo.
Juma lililopita kitengo cha chakula cha umoja huo,kililazimika kupunguza kiwango cha misaada ya chakula kwa wakimbizi wa Syria kutokana na ukosefu wa misaada ya kibinadamu.
Inaarifiwa kwamba kiasi cha dola za kimarekani bilioni kumi na tatu kilichoombwa na umoja wa Mataifa kwa mwaka huu wa 2014 hawakupewa zote.
0 comments:
Post a Comment