Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Tuesday, October 21, 2014

SOKA FELLAN NA BLIND WAIOKOA MAN UNITED DIMBAN "The Hawthorns'

KWENYE Mechi ya Ligi Kuu England ambayo Manchester United walitawala walijikuta mara mbili wakitoka nyuma na kusawazisha na kupata Sare ya 2-2 walipocheza Ugenini huko The Hawthorns dhidi ya
 West Bromwich Albion
FELLAN AKISHANGILIA BAO NA KAPTEIN MSAIDIZI  MAN U VAN PERSIE

Stephane Sessegnon aliipa WBA Bao katika Dakika ya 8 kwa kigongo kikali baada ya Kipa wao Boaz Myhill kupiga ndefu mbele kwa Andre Wisdom ambae alimsogezea Nahodha huyo wa Benin ambae Wiki iliyopita walikuwa Dar es Salaam na kufumuliwa 4-1 na Taifa Stars.
Hadi Mapumziko WBA 1 Man United 0.
Kipindi cha Pili Man United walianza kwa kumtoa Ander Herrera na kumwingiza Marouane Fellaini ambae aliwapa manufaa makubwa kwa kusawazisha kwa Bao safi katika Dakika ya 48 na hilo ni Bao lake la kwanza kwa Man United katika Ligi.
Lakini udhaifu wa Difensi ya Man United, wakati wakiwa wanatawala Gemu, uliwapa WBA mwanya mkubwa kupiga Bao la Pili Dakika ya 66 kupitia Saido Berahino.
Man United waliweza kusawazisha Dakika ya 87 baada ya Krosi ya Rafael kuokolewa na kumkuta Daley Blind aliepiga kiakili kufunga.
Sare hii imewaweka Man United Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Chelsea ambao Jumapili ijayo watatua Old Trafford kuivaa Man United katika mtanange unaongojewa kwa hamu.
VIKOSI:
WEST BROM: Myhill, Wisdom, Dawson, Lescott, Pocognoli, Gardner, Morrison, Dorrans, Sessegnon, Brunt, Berahino
Akiba: Ideye, Anichebe, Gamboa, Luke Daniels, Mulumbu, McAuley, Blanco.
MAN UNITED: De Gea, Rafael Da Silva, Phil Jones, Marcos Rojo, Luke Shaw, Daley Blind, Ander Herrera, Angel Di Maria, Juan Mata, Adnan Januzaj, Robin van Persie
Akiba: Falcao, Smalling, Lindegaard, Carrick, Young, Fletcher, Fellaini.
REFA: Mike Dean
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA-Mechi zijazo:
**Saa za Bongo
Jumamosi Oktoba 25
1445 West Ham v Man City
1700 Liverpool v Hull
1700 Southampton v Stoke
1700 Sunderland v Arsenal
1700 West Brom v Crystal Palace
1930 Swansea v Leicester
Jumapili Oktoba 26
1630 Burnley v Everton
1630 Tottenham v Newcastle
1900 Man United v Chelsea
Jumatatu Oktoba 27
2300 QPR v Aston Villa

DONDOO MUHIMU:
-Kabla ya Mechi hii, Man United hawajafungwa katika Mechi 8 za Ligi Kuu England na WBA Uwanjani The Hawthorns wakishinda Mechi 7 na Sare 1.

CREDIT:SOKA NI BONGO

0 comments: