Mtu aliyekuwa akitafutwa na jeshi la
polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya ya ulipuaji mabomu
kwenye maeneo mbalimbali jijini humo ameuwawa kwa kupigwa risasi na askari
polisi.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha
Liberatus Sabas amesema mtuhumiwa huyo ameuwawa usiku wa kuamkia leo baada ya
kupigwa risasi na polisi alipofanya jaribio la kutoroka akiwa chini ya ulinzi
akipelekwa wilayani Kondoa mkoani Dodoma.
0 comments:
Post a Comment