Shirikisho la mchezo wa soka duniani Fifa, limewasimamisha kwa muda wajumbe wawili wa kamati kuu, Mohamed Bin Hammam na Jack Warner baada ya kikao cha kamati yake ya maadili siku ya Jumapili.
Shirikisho hilo sasa litaanzisha uchunguzi kamili juu ya madai kwamba wajumbe wa shirikisho la soka la Caribbean walipewa rushwa.Mohamed Bin Hammam na Jack Warner |
Lakini rais wa Fifa Sepp Blatter hakupatikana na hatia yoyote.
Hata hivyo, Fifa imesisitiza kuwa hawana hatia kwa sasa hadi itakapothibitishwa kuwa walihusika katika sakata hilo.
SEPP BLATTER |
Bin Hammam alikuwa mpinzani pekee wa Blatter katika uchaguzi ujao wa urais wa Fifa lakini alijiondoa mapema siku ya JANA.
0 comments:
Post a Comment