CHECK me!!!!
Friday, December 29, 2017
Monday, October 2, 2017
Mauaji Las Vegas: Update kufikia sasa kuhusu shambulio Marekani
Mzee wa miaka 64 aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wanahudhuria tamasha ya muziki na kuwaua watu zaidi ya 58. Watu wengine 515 wanauguza majeraha.
Mshambuliaji alijipiga risasi, polisi wanasema.
Kulitokea nini?
Watu takriban 22,000 walikuwa wanahudhuria tamasha ya muziki wa country usiku wa Jumapili katika eneo la wazi karibu na uwanja mdogo wa ndege wa Las Vegas.
Milio ya kwanza ya risasi ilisikika mwendo wa saa nne usiku saa za Las Vegas (05:00 GMT).
Mshambuliaji aliwafyatulia watu risasi kutoka ghorofa ya 32 katika hoteli ya Mandalay Bay na baadaye akajiua kwa kujipiga risasi.
Taarifa za awali zilikuwa zimesema kuwa aliuawa na polisi
Walioshuhudia wanasema mamia ya risasi zilifyatulia na kwamba walisikia milioni ya bunduki za rashasha.
Kuliibuka mtafaruku na watu walikimbia huku na kule uwanjani wakijaribu kujificha.
Polisi wanasema kwamba taarifa kuwa kulikuwa na ufyatuaji wa risasi katika maeneo mengine ya uwanja wa ndege wa Las Vegas zilikuwa za uongo.
Mshukiwa ni nani?
Polisi wamesema wanaamini Stephen Paddock mwenye umri wa miaka 64 ndiye aliyehusika.
Hata hivyo, hawajasema chochote kuhusu nia ya mauaji hayo.
Mkuu wa polisi Joe Lombardo amesema maafisa wa polisi walipata hadi bunduki 10 katika chumba chake.
"Hatujapata maelezo yoyote baada ya uchunguzi au maelezo kumhusu mhusika huyo ambayo ni ya kukera (au kudokeza angetekeleza uhalifu)," Lombardo amesema.
"Jambo pekee tunaloweza kusema ni kwamba alitajwa katika kisa kimoja miaka michache iliyopita na kisa hicho kilishughulikiwa kama kisa cha kawaida katika mfumo wetu wa mahakama."
Maafisa wanaamini amekuwa hotelini humo tangu 28 Septemba.
Kakae Eric Paddock ameambia Reuters kwamba: "Hatuna habari zozote (kuhusu nia). Tumegutuka sana. Tumeshangazwa sana na tunatuma rambirambi zetu kwa jamaa za waathiriwa."
Kundi linalojiita Islamic State limedai kuhusika lakini halitajoa ithibati yoyote.
"Mshambuliaji huyo wa Las Vegas alisilimu miezi michache iliyopita," kundi la Islamic State limesema kupitia taarifa.
Kumetolewa wito wa kutafutwa kwa "mhusika mweingine" kwa jina Marilou Danley, 62, ambaye maafisa wanasema alikuwa anasafiri na mshambuliaji kabla ya kisa hicho kutokea.
Mwanamke huyo anaaminika kuwa alikuwa amesafiri nje ya Marekani.
Ni watu wangapi wameuawa?
Waliofariki wamefikia zaidi ya 58, kwa mujibu wa polisi.
Watu 515 wamepelekwa hospitalini wakiwa na majeraha.
Watu 14 wanaaminika kuwa katika hali mahututi, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
RAIS TRUMP AMESEMAJE?
Katika kituo na wanahabari White House, Rais Donald Trump amesema mauaji hayo ni "kitendo cha uovu".
Amewapongeza pia polisi wa Las Vegas kwa kuzuia mauaji zaidi, akisema walichukua hatua upesi sana.
Awali, rais huyo aliandika kwenye Twitter kuhusu shambulio hilo.
Ruka ujumbe wa Twitter wa @realDonaldTrump
My warmest condolences and sympathies to the victims and families of the terrible Las Vegas shooting. God bless you!— Donald J. Trump (@realDonaldTrump) 2 Oktoba 2017
Friday, August 18, 2017
Friday, August 4, 2017
kuongezeka kwa Wezi wa nywele za wanawake kwazua wasiwasi India
Zaidi ya wanawake 50 katia majimbo yaliyo Kaskazini mwa India ya Haryana na Rajasthan wamesema kuwa wmekatwa nywele zao wakati wakiwa hawana fahamu.
"Kulikuwa na mwanga mkali uliosababisha nipoteze fahamu. Saa moja baadaye niligundua kuwa nywele pia ikuwa imekatwa," alisema Sunita Devi, mwamamke mwenye umri wa miak 53 kutoka Haryana.
"Nemeshindwa kulala wala kufanya chochote. Nilisoma kuhusu visa hivi vikifanyika huko Rajasthan, lakini sikufikiria kingetendeka kwangu," aliongeza.
Mbali kidogo mwanamke mwingine Asha Devi naee alipoteza nywele yake katika shambulizi kama hilo siku iliyofuata.
Lakini wakati huo mshambuliaji aliripotiwa kuwa mwanamke.
Baba mkwe wake Asha Devi, Suraj Pal anasema kuwa kufuaia kisa hicho, alimshauri pamoja na wanawake wengine wa familia kuhamia nyumba ya jamaa wao kati jimbo la Uttar Pradesh.
Bwana Pal anasema alikuwa nyumbani wakati Asha Devi alitoka nje kufanya kazi zake.
"Nilienda nje kujua ni kwa nini hakurudi baada ya zaid ya dakika 30. Tulipata amapoteza fahamu katika chumba cha kuoga. Nywele yake ilikuwa imekatwa na kutupwa sakafuni."alisema.
Ripoti za kunyolewa wanawake kwanza ziliibuka mapema Julai kutoka jimbo la Rajasthan, lakini visa sawa na hivyo kwa sasa vinaripotiwa kutoka Haryan na hata mji mkuu Delhi.
Sunita Devi anaishi katika jamii ya wafanya biashara na wakulima.
Baadhi wa majirani zake wanachukua zamu kukaa naye hadi apate kuondokewa na mshutuko.
Anasema mshambuliaji wake alikuwa ni mwanamume mzee ambaye alikuwa amevaa nguo nyeupe.
Saturday, July 15, 2017
Breaking News: Matokea Kidato cha 6 Mwaka 2017 Yametoka..... Bofya hapa kuyatazama
Baraza la Mitihani la taifa (Necta) leo limatangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita.
Bofya hapo chini Kuyatazama
1. Matokeo ACSEE
2. Matokeo Ualimu (DSSEE)
3. Matokeo Ualimu ( GATSE)
Bofya hapo chini Kuyatazama
1. Matokeo ACSEE
2. Matokeo Ualimu (DSSEE)
3. Matokeo Ualimu ( GATSE)
Monday, June 26, 2017
rOCK D _tAWILE
BAADA YA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN,wasanii kibao wanatoa ngoma mpya ili kuendelea kuwapa Ladha mashabiki zao ila si kila nyimbo itakuwa na viwango bora hivyo kuna zile chache ambazo zinakidhi vigezo na hii ni moja wapo TOKA kwa msanii wa zouk Bongo Rock D amekuja na hii Tawile ISKIZE NA IPAKUE BURE
Thursday, May 11, 2017
Monday, May 8, 2017
Wednesday, March 29, 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)