Ice
cream ni kifunga hamu ya kula ( Dessert ) moja wapo nzuri sana na
inaweza kuliwa na watu wa lika zote pia unaweza kula ice cream muda
wowote ule utakaojisikia na ukafurahia hasa ukiangalia hali ya joto
inayopatikana nchini kwetu. Fata maelezo hapochini jinsi ya kutengeneza
pamoja na mahitaji ili ufanikishe uandaaji wako.
Vitu vya kuandaa.
Maziwa ml 240
Sukari ml 240
Chumvi kijiko kidogo cha chai robo (1/4)
Vanilla ya maji kijiko kikubwa cha chakula 1/2
Vanilla ya mti ml 120
Low fat maziwa ml 120
low fat cream ml 120
Whipping cream yenye ubaridi wa wastan ml 480
Biskuti zilizochovywa Chocolate cream ml 480
Badala ya biskuti zilizochovywa na
chocolate cream unaweza weka vipande vya chocolate, unaweza weka
mchanganyiko wa ladha mabalimabli mfano matunda kama strawbery, cherry,
Embe kwa kuchanganya kiasi cha ml 480 kama inavyoonyehs hapo juu katika
mtiririko wa vitu vya kuandaa.
Vunja vunja vipande vya biscuti vilivyochovywa na chocolate weka pembeni safi ukisubiri baadae kidogo kuzitumia.
Weka
maziwa katika sufuria nzito kwenye jiko lenye moto wa wastan acha
yachemke pole pole mpaka yatakapotoa mapovu pemebi ya sufuria yatoe na
weka pembeni yapoe.
Baada ya kutoa maziwa katika moto na kuyaweka pembeni yapoe changanya sukari na chumvi ndani yake
Koroga vizuri maziwa hayo mpaka sukari na chumvi viyeyuke vizuri
Changanya
tena whiping cream na vanillah kwenye maziwa yale pole pole kisha
changanya maziwa na ile cream vilivybaki ambavyo vyote vinamafuta kiasi (
low fat ) mpaka ichanganyike vizuri.
Kisha mimina mchanganyiko wako wote kwenye bakuli safi la kioo ili uweze kupoa na kuganda
Baada
ya kumimina katika bakuli chukua bakuli jingine kubwa kiasi ya lile
lenye mchanganyiko wako kwajili ya kugandisha kua ice cream. Weka barafu
katika bakuli hilo kisha weka juu yake bakuli lenye mchanganyiko
wako. Baada ya mchanganyiko wako kupoa kabisa chukua plastic wrap funika
bakuli lako vizuri na weka katika friji kwa masaa 4 au hata masaa 24
kwa kuweka mchanganyijo wako ndani ya friji itasaidia sana kubadilisha
mchanganyiko kua rojo rojo au mzito na inakua rahisi kukoroga tena ili
upate umbile halisi la ice cream na laini kwa mlaji.
Baada ya masaa 4 au masaa 24 toa mchanganyiko wako kwenye friji kisha koroga vizuri na mwikosafi wa mbao au kijiko kikubwa.
Kisha
funika tena na plastic wrap au foil kitu chochote kitakachozui hewa
kuingia katika bakuli lako tayari kwa kugandisha kwenye freezer. Baada
ya hapo weka bakuli lako katika freezer na ruhusu mchanganyiko wako ukae
kwa masaa 2 kwenye freezer kisha utoe.
Baada
ya kutoa mchanganyiko wako katika freezer tumia mashine ya kuchapia au
unaweza tumia mchapo wa chuma au unaweza tumia uma ya kulia chakula na
kukoroga vizuri mchanganyiko amabao utakua tayari umeshaanza kuganda
lengo ni kuvunjavunja mapande ambayo yameshaanza kuganda. Kisha funika
na plastic wraptena na rudisha katika freezer kwa masaa 2.
Baada
ya masaa 2 toa mchanganyiko wako na koroga kwa kutumia mashine au uma
yakulia chakula. Ice cream yako itakua nzito safi lakini bado kwa kuweza
kuchota na kuliwa, kama mchanganyiko bado haujaganda vizuri kutokana na
nguvu ya freezer rudisha kwenye freezer igande tena kwa muda kiasi.
Baada
ya ice cream yako kua imeganda vizuri chukua zile bisckuti zenye
chocolate tupia katika mchanganyiko wako wa ice cream na uchanganye
vizuri sana kwa umakini, aidha inaweza kua ni matunda ya ladha yeyote
badala ya biskuti bado itapendeza na utakua umebadilisha ladha.
Kisha
chukua chombo cha plastic kisafi na kikavu, weka mchanganyiko wako
ndani yake na hakikisha unaacha nafasi ya inchi 1 au 1/2 inchi kwajili
ya kutanuka.
Kisha funika vizuri plastic yako na mfuniko safi na uirudishe katika freezer iweze kuganda kabisa mpaka itakapokua ngumu.
Baada
ya ice cream kua ngumu toa kwenye freezer fungua chombo chako cha
plastik na tumia chombo maalumu cha kuchotea ice cream vipo vingi sana
hapa nyumbani tanzania vinauzwa kwenye supermaket. Chota maumbo mazuri
sana ya mviringo kisha weka kwenye bakuli au glasi ya udongo na ufurahie
ice cream yako!!
NATUMAI MPAKA HAPO MTAKUA MMEELEWA VIZURI SANA SOMO HILI LA LEO NA KUWEZA KUTENGENEZA ICE CREAM SAFI KABISA WATOTO, BABA AU MGENI AKAFURAIA SANA CHAKULA HIKI CHEPESI.
NAOMBA
MTENGENEZE KWAKUFATA MAELEKEZO VIZURI HALAFU MNIPATIE MATOKEA KISHA
TUENDELEE NA SOMO BAADA YA KUTENGENEZA ICE CREAM HIYO UTAIPAMBA VIPI
TUTAFANYA UPAMBAJI WA AINA TOFAUTI ZENYE LADHA MBALIMBALI YA ICE CREAM
AINA 10 HADI 20.
0 comments:
Post a Comment