Utafiti umefanywa na wanafunzi
wa University of Nottingham Uingereza ukihusisha nchi 159, wanafunzi wa
chuo kikuu cha Nottingham wamefanya utafiti wa kugundua ni nchi zipi
zinaoongoza kwa uaminifu au ukweli duniani, utafiti umefanywa ukihusisha
nchi 159 ikiwemo Tanzania.
Wanafunzi hao wamefanya tafiti huku
wakichanganya na data za 2003 za ukwepaji kodi, rushwa na udanganyifu
katika siasa lakini wamegundua kuwa nchi za Lithuania, Uholanzi,
Uingereza, Sweden, Ujerumani na Italia zimetajwa katika list ya nchi
zinazoongoza kwa uaminifu.
Wakati
nchi za Tanzania, China, Uturuki, Poland na Morocco zimetajwa kuwa ni
miongoni mwa nchi zinazoongoza watu wake kutokuwa waaminifu, utafiti huo
unaeleza kuwa watu wanaoishi katika nchi zenye rushwa na siasa za
udanganyifu wamekuwa sio waaminifu au wakweli, wakati watu wanaotokea
katika nchi ambazo hazina rushwa na ukwepaji kodi ni waaminifu.
Tafiti zimefanyika katika chuo kikuu cha Nottingham
Uingereza, lakini kimetajwa kufanya majaribio kwa kuhusisha
vijana 2,586 wenye wastani wa umri wa miaka 22 kutoka nchi 23
zikiwemo Vietnam, Morocco, China, UK, Hispania, Sweden, Italy na Czech Republic. Utafiti huu umetolewa na dailyamail.co.uk March 11 2016.
IMEANDIKWA : dailymail.co.uk
0 comments:
Post a Comment