Na Ripota wa Sufianimafoto ,Dar
UKIHADITHIWA na kuonyeshwa chumba cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa amepiga pamba wala hutaamini masikio yako wala macho yako pindi utakapopata bahati ya kufika na kushuhudia chumba hicho kilichopo maeneo ya Gold Star Mtaa wa Mbezi Mtoni Bondeni jijini Dar es Salaam.
UKIHADITHIWA na kuonyeshwa chumba cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa amepiga pamba wala hutaamini masikio yako wala macho yako pindi utakapopata bahati ya kufika na kushuhudia chumba hicho kilichopo maeneo ya Gold Star Mtaa wa Mbezi Mtoni Bondeni jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa habari hii alipata
fursa ya kufika na kushuhudia yale yaliyokuwa yakisemwa na baadhi ya
wakazi wa mtaa huo jana majira ya saa tano usiku baada ya kutokea
mtafaruku na sintofahamu katika nyumba hiyo ya Mama Mwakajinga,
anayoishi Dereva huyo aliyejulikana kwa jina la Steven al-maarufu kama
‘NYATI’.
Akizungumza na mwandishi kuhusu tukio hilo,
Mama mwenye nyumba, alisema kuwa siku ya Mei 23, akiwa ameketi uwaji
karibu kabisa na Chumba cha Jamaa huyo huku akichambua mboga, alihisi
harufu kali na mbaya iliyokuwa ikivuma kutoka chumbani kwa Dereva huyo
aliyepanga katika nyumba yake tangu mwaka 2008 na kuona wadudu aina ya
funza wakitoka chumba hicho kupitia chini ya mlango.
Kesho yake Mei 24 baada
ya kuona wadudu hao huku harufu ikizidi kuwa kali, alimuita jirani yake
na kumshirikisha jambo hilo huku wote wakishikwa na butwaa na kuwa na
mashaka na chumba hicho.
Mei
25 Mama mwenye nyumba aliamua kwenda kwa Mjumbe wa eneo hilo Badili
Makoye, kutoa taarifa juu ya wasiwasi uliotanda katika nyumba hiyo na
kuongozana na Viongozi wengine, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo,
Frank Kyaruzi, Wajumbe wengine Abdalla Mlaliya na Matrida Paston,
waliofika na kujionea hali halisi ya chumba hicho.
Baada
ya viongozi hao kufika eneo la tukio walimuamuru Mama mwenye nyumba
kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi. Mama huyo alitekeleza agizo na
kwenda kuripoti Kituo cha Mbezi Garden na kuongozana na Mkuu wa Kituo
hicho na baadhi ya askari hadi nyumbani na kukuta hali hiyo ya
sintofahamu.
Walipofika
eneo la tukio na kushuhudia hali hiyo, Mkuu wa Kituo aliamuru mlango
huo uvunjwe huku wananchi na Viongozi wa Mtaa huo wakishuhudia na
kuingia ndani ambako walikuta Chumba kizima kikiwa kimejaa Chupa za
Plastiki zilizojaa mikojo, Mifuko ya Rambo ikiwa na Vinyesi, Feni moja
iliyochomekwa kwenye Soketi ya Umeme ukutani, Pakiti nyingi tupu za
Sigara aina ya Embassy na Kondomu zilizotumika na zisizotumika.
Baada
ya zoezi hilo, Mwenyenyumba alimpigia simu mpangaji wake na kumtaka
kurejea nyumbani, lakini Dereva huyo alijibu kuwa kwa muda huo alikuwa
mbali maeneo ya Kunduchi na kuahidi kuwagongea usiku pindi atakaporejea.
Hadi Mwandishi anaondoka
eneo la tukio majira ya saa tano usiku bado wakazi wa maeneo hayo
walikuwa wamejazana nje ya Chumba hicho wakiendelea kumsubiri arudi ili
kupata ukweli kuhusu mambo waliyoyaona katika chumba chake.
Aidha Mama mwenye nyumba alisema kuwa
mpangaji wake huyo, tangu alipohamia katika nyumba hiyo mwaka 2008,
hakuwahi kumuona akiingia na mwanamke katika chumba hicho, wala kumuona
mgeni wa aina yeyote kwa Dereva huyo,jambo lililomshangaza kukuta Kondom
zilizotumika katika chumba hicho. Ama kweli ukistaajabu ya Mussa
utayaona ya Filaun.
Leo
hii Mei 27, Mama mwenye nyumba ameripoti kuwa mpangaji wake
huyo,hajatokea nyumbani hapo tangu kutokea kwa tukio hilo ambapo leo,
amechukua uamuzi wakuwalipa vijana wa mtaa huo ili wasafishe chumba
hicho.
Wananchi na mwenye nyumba wakifungua mlango
Chupa zinazodaiwa kuwa na mikojo zikiwa zimetapakaa ndani ya chumba hicho.
Huyu Ndiye Dereva wa Tax Nyati anayedaiwa kumiliki chumba hicho.
0 comments:
Post a Comment