Wanakwambia hayawi hayawi sasa yamekuwa Di Maria afungua ukurasa mpya na PSG
Naandika barua hii kuishukuru familia nzima ya Manchester United kwa kuniunga mkono kwa mwaka mmoja niliokuwa sehemu ya klabu.
Manchester United
waliponichagua kuwa sehemu ya timu yao, nilijisikia kuheshimiwa
kwasababu nilijua klabu hii ina maanisha nini na jinsi gani iliniamini.
Hata hivyo, nafahamu mambo hayakwenda vizuri kama tulivyotarajia, naomba msamaha kwa hilo.
Katika maisha ya mcheza mpira, kuna wakati mwingine mambo usiyotarajia na usiyoyataka yanatokea.
Nawahakikishia kwamba haikuwa
kujaribu. Nilijitahidi niwezavyo, lakini mpira sio kama hesabu: Mara
zote kuna vitu vingi vinavyoathiri vile unavyofikiria.
Samahani sana kwasababu sikufanya kile nilichotarajia katika klabu hii kubwa na ya ajabu.
Natoa shukurani za pekee kwa
bodi ya wakurugenzi na utawala ya Manchester United, vilevile kila
kiongozi na wachezaji wenzangu walioniunga mkono.
Pia shukurani za pekee ziwaendee mashabiki ambao mara zote waliniamini na kuonesha heshima na mapenzi makubwa.
Sasa ni wakati wa kujiunga na PSG, lakini Utukufu wa Manchester United utabaki kwenye kumbukumbu zangu daima.
Nawatakia kila la kheri
Angel di Maria.
0 comments:
Post a Comment