Wanasayansi
kutoka Marekani wana imani kuwa sokwe wana uwezo na akili ya kupika
chakula. Wanasayansi hao wamefanya baadhi ya majaribio ambayo
yameonyesha kuwa sokwe wanaweza kupika mboga za majani na wana uwezo wa
kuhimili kusubiri chakula cha moto.
Hata kama wanyama wengi wana
desturi ya kula chochote wanachokipata na kula moja kwa moja. Watafiti
kutoka chuo kikuu cha Harvard wanasema matokeo ya utafiti walioufanya
unasema kuwa Sokwe wana uwezo wa kupika na inawezekana suala hili
liligundulika muda mrefu uliopita.Hivyo wanachokihitaji sokwe ni ujuzi wa upishi kwani imedhihirika kuwa wana uwezo wa kuhimili moto.
0 comments:
Post a Comment