Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Wednesday, June 10, 2015

baada YA KUDAIWA KUTEMBEA NA MPENZI WA LINAH,WEMA AMPIGA MADONGO MSANII HUYO


Imelda Mtema
NI shiida! Siku chache baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’ kulalamika juu ya kitendo cha Wema Sepetu ‘Madame’ kumchukua aliyekuwa bwana’ake Nangari Kombo, muigizaji huyo ameibuka na kutoa maneno yanayoashiria kejeli, kuwa aache presha, kwani zile ni picha tu!

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madame'.
Katika gazeti la Risasi Jumamosi, toleo lililopita, iliripotiwa na kuchapishwa habari na picha zilizomuonyesha Madame akiwa amepozi kitandani na kijana huyo, aliyepata umaarufu baada ya kuingia ndani ya eneo la kuchezea katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam mwaka 2010, wakati wa mechi kati ya Brazil na Taifa Stars na kumkumbatia kiungo nyota wa mabingwa hao wa zamani wa dunia, Kaka.
Lakini Risasi Mchanganyiko lilipotaka kujua maoni yake juu ya shutuma hizo, Wema alisema kupiga picha na Nangari hakumaanishi mapenzi, kwani yeye ni mtu wa watu na picha kama hizo hupiga na marafiki zake wengi tu, hivyo Linah asiwe na shaka naye hata kidogo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Esterlina Sanga ‘Linah’.
“Nilipiga naye kama ninavyoweza kupiga na marafiki wengine kama akina Martin Kadinda, Petit Man na wengineo. Sina uhusiano naye wa kimapenzi, naomba aamini kuwa ni rafiki tu wa kawaida,” alisema Wema na kuibua maswali juu ya aina ya uswahiba wa kawaida wa kupiga picha kitandani na mpenzi wa mtu!



Related Posts:

0 comments: