Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Monday, June 22, 2015

Asili na historia ya neno la picha ya mnato ya "SELFIE" _CHEKI MABABU WA ZAMANI WALIVYOKUWA WANAJIPIGA SELFIE NI NOMA

Karibu kila mtu duniani leo hii

analijua neno “Selfie” ambalo maana yake ni picha ya mnato ya kujipiga mwenyewe
kwa kujielekeza Camera, lakini ni wachache wanaojua kwamba neno hilo lilianza
kuvuma muda wa mwaka juzi tu, pale watunzi wa kamusi za Oxford walipoliweka kwenye
kamusi zao na kulitaja kuwa ndilo neno la mwaka 2013 na kulipa maana hiyo ya kujipiga picha mwenyewe na kutundikwa kwenye
mitando ya kijamii.


Ingawa matumizi ya neno “Selfie”
linaonekana ni la kileo, lakini tendo la mtu kujipiga picha mwenyewe si  geni kabisa kwani tangia miaka ya awali ya
sayansi ya picha za mnato aghalabu watafiti na waendelezaji wa sayansi hii
walizoea kujipiga picha wenyewe katika kufanikisha tafiti zao. 


Hapo elewa
kwamba sayansi hii ilianza tokea miaka ya 1800 mwanzoni na katikati ya miaka
hiyo na kuendelea





Hiyo hapo juu ndiyo “Selfie”
inayoaminika kuwa ni ya kwanza kabisa kupigwa duniani na kuwepo katika kumbukumbu iliyopigwa
mwaka 1839 na mkemia na mtafiti wa picha za mnato aitwaye Robert Cornelius wa
jiji la Philadelphia nchini Marekani



Akitumia mbinu zilizotumia
wakati huo, huyu bwana alijipiga picha hii kwa kufunua lensi (zamani hakukuwa
na kitufe cha kubofyea, ilikuwa unafunua lensi kwa muda maalumu na kisha
kuiziba) na akaenda mbele ya Camera ambako alikaa kwa muda unaotakiwa lensi
kuwa wazi, kisha akarudi na kuiziba. Nyuma ya hii picha akaandika  “The first light Picture ever taken. 1839.”
 Yaani “Picha ya mwanga ya kwanza kabisa
kuchukuliwa. 1839”





nimefanya utafiti
huu wa kubaini picha moja ya mnato ya watu wanne wanaojipiga "Selfie" mwaka 1920  (HAPO CHINI) inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii   na kudaiwa kuwa ndiyo “Selfie”  ya  awali kabisa .

 


Hivyo ukweli ndio huo hapo juu.

0 comments: